Maisha yanaogopesha ila wewe usiogope

Maisha yanaogopesha ila wewe usiogope

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
34,281
Reaction score
79,891
MAISHA YANAOGOPESHA ILA WEWE USIOGOPE.

Na, Robert Heriel.

Nazo siku zaenda hata hazirudi tena. Siku huja kwa furaha nazo zaondoka kwa huzuni. Huja na Nuru kisha huondoka na giza. Nazo zaja na watu wake na kuondoka na Watu wasiowake.

Nayo maisha ya mwanadamu yamejaa dhiki na taabu. Yamejaa udhalimu na dhuluma. Mioyo yao imejazwa ubinafsi na uchoyo.
Lakini sikia ee mwanangu jiepushe na uovu. Jitenge na wenye dhambi nawe utasalimika.

Usiyaogope maisha ingawa yanaogopesha. Usiiogope kesho ijapokuwa huijui.

Nawe utakapokuwa na akili. Utakapoanza kutembea huku na huko duniani. Utakutana na mambo yatakayoutisha moyo wako. Mambo yatakayo uhuzunisha moyo wako. Basi usihuzunike wala kuogopa kwa maana Mungu wa Baba yako atakuwa pamoja nawe.

Nawe utakapo balehe, hisia zako zitakapoanza kuchemka. Ikiwa weww ni Binti yangu, au mwana wangu wa kiume. Utakutana na vijana wazuri kukushinda. Vijana wazuri kwa sura. Tena warefu kukushinda. Vijana watanashati. Wenye pesa na elimu kukushinda. Tena Wenye vyeo na vijana maarufu.

Usiwahofie wala usiwaogope ikiwa mtaingia kwenye hali ya kugombania Mchumba wa kuoa. Usiusikilize moyo wako bali sikiliza akili yako. Akili yako iutiishe moyo wako.

Wala usiseme moyoni mwako; tazama mimi si mzuri wa sura, tena sio mrefu, nisiye na pesa wala cheo. Mimi sio kitu. Siwezi kupambana na Vijana hawa wazuri na wenye kila sifa njema.

Kamwe usije sema hivyo. Wala usiwaogope vijana hao. Bali ishike sana sheria ya Baba yako aliyokupa. Mche Mungu sana kwa maana yeye ndiye atakayekushindia.

Tena wao wamepambwa kwa nje lakini wewe umepambwa kwa ndani. Wao wananguvu nje lakini wewe unanguvu ndani. Usiwaogope. Utafanya kama niliyokuambia naye hiyo binti atakupenda.

Kamwe usijisikie duni kwa vile uonekanavyo, au usemavyo ikiwa ndivyo ulivyozaliwa. Ikiwa umeumbwa kwa ukamlifu wa mtu mwenye kuonekana anamapungufu. Usiyasilikilize maneno yao wala usiusikilize moyo wako ikiwa utapotoka.

Nawe utaenda kwenye Harusi au misiba, au mahafali au maulidi au sherehe yoyote ile. Huko huenda utaona watu waliovaa kupenda zaidi yako. Waliovaa nguo za gharama. Tena wenye magari ya kifahari lakini wewe huna gari. Usiogope wala kujisikia vibaya mwanangu.

Tena kama utakuwa na mke wako au mume wako. Usimdharau mkeo/mumeo kwa sababu hajapendeza kama wao. Wala usijidharau mbele ya mumeo au mkeo kwa sababu hujapendeza kama wengine. Usiogope kwa kuwa Mungu wa Baba yako anakuona naye atakupa kwa wakati wako. Kikubwa usisahau sheria nilizokuamuru Mimi Baba yako.

Usiogope siku ukienda kutafuta elimu. Iwe ni mashuleni au Katika Vyuo. Huko utakutana na vijana waliosomea shule zenye viwango vikubwa. Hao usiwaogope. Tena utakutana na vijana wenye muonekano wa akili. Pia hao usiwaogope. Utawaona wenye Kujipamba wakapambika ilhali wewe huenda usiwe na uwezo huo. Usiwaogope. Mche Mungu na kuzishika sheria zake. Ishi kwa kumpenda yeye nawe utakuwa mtu mkubwa mahali hapo. Watakuogopa usemapo. Wakuogopa utembeapo. Watakuogopa ukaapo na ulalapo. Kwa maana unashika ile siri niliyokupa. Maisha yanaogopesha ila wewe usiogope.

Nawe utaenda kuomba kazi. Huenda ukawa huna watu uwajuao watakao kusaidia kupata kazi. Huenda usiwe mzuri kwenye lugha wakati wa usaili wakati wengine wapo vizuri kwenye lugha. Huenda siku hiyo utakayoenda kusailiwa ukaona wenzako wakija na magari au wakiletwa na magari wakati wewe miguu yako imejaa vumbi. Usifadhaika moyoni mwako wala usihuzunike. Jikaze kama mwanaume kwa maana muda wako unakuja. Mungu ndiye atakayekupa hitaji la moyo wako. Ikupasayo ni kumcha yeye.

Nawe utaona wenzako wakiolewa wakati wewe umri unaenda na dalili hazionekana za kuchumbiwa. Usiogope maisha hata ukamuacha Mungu wa Baba yako. Mungu ndiye ajuaye mchumba sahihi kwako. Ndiye ajuaye wakati sahihi wa wewe kuolewa. Unachopaswa ni kulinda Bikra yako mtu asiiguse tena usirihusu kijana akufunue kama sio mume wako. Ndipo utakapoitwa Mama mbarikiwa. Nao watoto wako watakuwa baraka kwako na kwa ulimwengu.

Usiogope wengine wakijenga majumba makubwa ilhali wewe huna mbele wala nyuma. Jipe moyo nawe kazana mpaka Mungu akuone. Fanya kazi kama alivyoagiza. Kamwe usiruhusu uvivu utawale maisha yako. Fanya kazi yoyote ile naye Mungu atakuinua. Utakuwa juu kama Mungu wa Baba yako alivyokuwa juu. Usiwaogope hata kama unadhani wanaogopesha.

Usijisikie duni mbele ya mtu yeyote yule. Popote ulipo Mungu wa Baba yako yupo. Jisikie fahari na jiamini popote pale ulipo. Haijalishi unaonekanaje. Hajalishi unaelimu ipi. Haijalishi unatokea Familia gani. Usiogope mtu yoyote ingawa unaweza dhani wanaogopesha.

Usiogope hata kama upo mikononi mwa adui. Maisha yanaogopesha kwa vile waovu ndio wametamalaki lakini wewe usiogope ikiwa unatetea haki. Waambie ukweli na simamia haki siku zote za maisha yako. Nao watakuogopa.

Usiogope pale uendapo vitani. Huenda adui zako wakawa na silaha kali na kubwa kukushinda. Huenda wakawa na jeshi kubwa kukushinda. Huenda wakawa na miili mikubwa kukushinda. Hata waweje kamwe usiogope hata kama wanaogopesha kwa maana Mungu wa Baba yako ananguvu kuwashinda. Naye atawapiga kwa silaha zao walizozibeba. Usiogope maisha.

Maisha yanaogopesha sana ila wewe usiogope. Yanaogopesha kwa kuwa wapo wenye nguvu kukushinda. Wapo wazuri na wenye akili kukushinda. Wapo wenye Mali na utajiri kukushinda. Wapo wenye Wake na watoto wazuri kukushinda. Lakini Ukimcha Mungu niliyekuagiza watu hao wote watakuogopa.

Usiogope ikiwa siku moja utakutwa na Maradhi na ugonjwa mkali au wa aibu. Bali wewe mche Mungu wa Baba yako. Usihofie kesho yako kwa kuwa Mungu wako ndiye aijuaye.

Lakini najua wewe ni mwanadamu tuu. Nawe ni kiumbe dhaifu. Basi ikiwa hofu itakushinda basi Usisahau kusoma kile kitabu nilichokuandikia. Naam kitabu cha Baba yako.

Nawe utakapokutwa na jambo la dharura. Iwe ni msiba. Iwe ni ajali mbaya. iwe ni jambo lolote basi usihofu kwa kuwa Mungu wa Baba yako ndiye mwenye jukumu la kukusaidia wala hapana mwingine awezaye kukusaidia isipokuwa yeye. Mtumainie. Nawe utamuomba kama nilivyokufundisha.

Basi nimalize kwa kusema. Dunia inazunguka. Yajiviringa viringa lakini macho ya wanadamu hayaoni. Hawaoni Bwana, Mungu wetu atembeapo. Hasikii Mungu wetu asemapo kwa kuwa masikio yao yametiwa uziwi. Nayo macho yao yametiwa upofu. Lakini wewe Utaona visivyoonwa. Utasikia visivyosikiwa. Utafikiri visivyo vikifiriwa. Utafanya visivyo fanywa. Kwa maana Umemcha Mungu wako.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi.
0693322300
 
Tbt
 
Taikoni noma sana

Madini ya kishindo
 
FAIDA ZA VIFURUSHI VYA T!G∅ POSTPA!D.

1. GB NYINGI PESA KIDOGO.

2. UKISHAPEWA KIFURUSH MWEZI WA KWANZA MIEZ INAYOFUATA KILA TAREHE 1 UNAPEWA KIFURUSH KISHA UNALIPIA SIKU UOYOTE UKIWA NA HELA

3. UNAPEWA KIFURUSHI KISHA UNAWEZA KULIPIA KIDOGO KIDOGO KIFURUSH ULICHOCHUKUA.

4. VIFURUSHI VINADUMU MWEZI MZIMA NA KINAJIRUDIA KILA TAREHE 1 KWA MIEZ 24.YANI MIAKA MIWILI YOTE.

5. UKIWA NA DENI LA NIWEZESHE, UKIJIUNGA HUDUMA HIZI DENI LINASAMEHEWA.

6. KUNA USALAMA UNAPOJIUNGA HUWEZI KUTAPELIWA NA MTU MANA MALIPO UNAFANYA YANAENDA T!G∅ MOJA KWA MOJA, HUMTUMII MTU YOYOTE HELA.

7. MKIWA WATU WA5 AU ZAID MNAPEWA OFFER YA KUWASILIANA NYIE KWA NYIE BUREE BILA KUKATWA CHOCHOTE YANI HATAKAMA UNA SALIO 0 NA DAKIKA 0 UNAMPIGIA MWENZAKO MNAONGEA MUDA WOWOTE.

MCHANGANUO

15000 UNAPATA 15GB KILA MWEZI.

30000 UNAPATA GB 35 KILA MWEZI.

40000 UNAPATA GB 48 KILA MWEZI.

60000 UNAPATA GB 72 KILA MWEZI

100000 UNAPATA GB 120 KILAMWEZI

NJOO NIKUPE MAELEKEZO BURE UJIUNGE MWENYEWE.

KAMA NILISHAWAHI KUKUUNGA NILETEE WENZAKO NDUGU MARAFIKI WAJIUNGE THEN NIKULIPE.

NICHEKI WHATSAPP 0717700921 una swali karibu!!kiakili la Kheri
 
Back
Top Bottom