Maisha ya Papa mpya

Maisha ya Papa mpya

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,037
Reaction score
34,741
papa_miguu.jpg
Papa Francis I wakati akiwa Kardinali wa Buenos Aires akiendesha ibada ya kuosha miguu (Alhamisi Kuu), mwaka 2005, nchini Argentina. Picha na AFP

KWA UFUPI
Aliishi maisha ya kawaida kwa kutumia usafiri wa umma, kujifulia, kujipikia, kusaidia wagonjwa na wasiojiweza

Vatican City, Vatican. Siku moja baada ya kuchaguliwa kuliongoza Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis 1 anaelezwa kuwa aliishi maisha ya kawaida akiwa Askofu Mkuu wa Buenos Aires Argentina, ambapo alijifulia nguo zake mwenyewe, kupiga pasi na kupika.
Kiongozi huyo pia alikuwa akitumia usafiri wa umma licha ya kuwa wadhifa wake uliruhusu kupewa gari la kifahari.


Katika shughuli zake, Papa Francis 1 alitumia usafiri wa basi la abiria kama daladala ambapo nchini Argentina ni maarufu kwa jina la “el micro.”
Katika kuonyesha unyenyekevu kwa watu wenye shida mbalimbali, Papa Francis alipenda sana kuwasaidia wagonjwa wa Ukimwi, wasiojiweza na waathirika wa matumizi ya dawa za kulevya.



Papa huyu ambaye ni wa kwanza kutoka Amerika, anawakilisha tamaduni mbili, akiwa mtoto wa wahamiaji waliotoka Italia kwenda kuishi Argentina.



Hata katika siku ya kwanza jana tangu achaguliwe kuwa Papa juzi, Francis 1 aliendesha ibada ya asubuhi na kisha kugoma kulipiwa bili yake ya hoteli kama njia ya kuonyesha uwajibikaji.

Kwa nini alijiita Francis?
Aliamua kuchukua jina la Mtakatifu Francis wa Assisi, ambaye aliamua kuacha mali na maisha ya kifahari kutoka kwa wazazi wake na kuanzisha Shirika la Kitawa la Ndugu Wadogo.
Mtakatifu Francis wa Assisi anakumbukwa kwa kuishi maisha ya umaskini, huku akijali watu wenye shida na wagonjwa.



Akimzungumzia Papa Francis, muda mfupi baada ya kuchaguliwa kuliongoza Kanisa Katoliki duniani, Mkurugenzi wa Habari wa Vatican, Padri Thomas Rosica alisema kuwa Baba Mtakatifu aliishi na kufundisha imani yake kwa watu aliowaongoza kama Padri, Askofu na Kardinali akiwa pia mtu wa sala.



Padri Rosica, ambaye pia ni msemaji wa Vatican katika lugha ya Kiingereza, aliwaambia waandishi wa habari katika mkutano aliouandaa akibainisha kuwa alizungumza na Papa Francis, Jumapili iliyopita.



“Jumapili usiku tulikuwa katika matembezi, alinishika mkono na kusema, ‘naomba uniombee. Nina mawazo mengi,”alisema Padri Rosica akimnukuu Papa Francis 1 na kuongeza kuwa alitimiza ombi hilo la Papa.



Alifafanua kuwa katika mazungumzo yao, Papa Francis 1 alimweleza kuwa amekuwa akiishi maisha ya kawaida nchini Argentina akiwa pia mlezi wa watawa wa Shirika la Majesuit walio wagonjwa.



“Nimeishi maisha ya kawaida katika makazi duni, nilikuwa mlezi wa watawa wasiojiweza wa Shirika la Majesuit nchini Argentina, nilipika mwenyewe na kutumia usafiri wa umma katika kazi zangu,” Padri Rosica alinukuu maelezo ya Papa katika mazungumzo yao.



Kwa upande wake, Padri Federico Lombardi wa Shirika la Majesuit alisema: “Nimeshtushwa na taarifa za mjesuiti kuchaguliwa kuwa Papa.”



Alisema kwamba ingawa hamfahamu vizuri Papa Francis 1 zaidi ya kukutana naye katika mkutano mkuu wa Majesuit , lakini kuna ishara ya wazi ya kichungaji na kiroho unapokutana na Papa Francis kwa mara ya kwanza.



“Sikutarajia, hii inaonyesha moyo kwa upande wa makardinali. Ni mara ya kwanza kupata Papa kutoka bara jingine kwa karne nyingi sasa,” alisema Lombardi.
http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1720538/-/128lo83/-/index.html

 
Mungu amtie nguvu kwenye shughuli zake za kitume,asa kipindi hiki ambapo kanisa lia majaribu mengi,waswahili tunasema mti wenye matunda ndio unapigwa mawe,so hatushangai watu mbali mbali na vyombo vingi vya habari vikiwa vinatafuta habari negative za ukatoriki na papa.
 
Back
Top Bottom