Maisha ya Ndoa

Bullshit

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
1,300
1,495
Mtaani kwetu marafiki zangu wananiambia nichukue jiko,
Nikiwa na mke nitafanikiwa.

Hivi kuna husiano gani wa mafanikio kwa mwanamke ndani ya ndoa.?

Hivi nini maana ya ndoa.
Majira zangu wananiambia mimi yawezekana s mwanaume kamili wengine wananiita muhuni.

Lakini hao hao wanaoniambia hivyo kila siku wake zao kunigongia mlango kuniambia matatzo ya waume zao.

Hao hao ambao wanajiona bora kwa vile wameoa kila siku wanaomba niwakopeshe hela ya matumizi ili wahudumie familia eti hali mbaya.

Watoto zao wanakuja kwangu niwatafutia ajira,na ninawasaidia katika mambo mengi.

Ila tu wamekuwa wanajiona bora kuliko mimi.
Ninapowaambia Ndoa sio kukurupuka!,uwa wananijibu,mwanamke uja na baraka,
Kuna mmoja niliwahi kumuambia unanishauri nioe na bado hela ya chakula nakupa mimi,alichukia mpaka leo alikata mawasiliano.

*hivi ni kweli kuoa ndo inamfanya mwanaume aitwe mwanaume?
*N kweli ukitaka ufanikiwe lazima uwe na mke?
*kuoa imeandikwa ni lazima?

nawakilisha.
 
Oa mtu unae elewana nae, usioe kwa kuwafurahisha marafiki oa kwakua uko tayari na ume pata mtu sahihi.

Hakuna formular ya maisha lakini vunja mifupa bado meno ipo hajawahi kumuangusha mtu.

Ukiona ukiwa kijana inakusaidia kutuliza akili, ukifika 50 unaweza kuwa na familia, maisha na bado una nguvu.
 
Maisha ya ndoa si ya kukariri na kamwe usikurupuke kuoa mana waweza juta maisha yako yote

Omba sana Mungu akupe mke mwenye akili za maisha na hofu ya Mungu mtakayependana mpaka mkazikana hapo ndio utaona utam wa ndoa

Kuwasaidia watu haimanishi labda watu walioko kwenye ndoa ndio wanakumbana na changamoto pekee hata wasiooa hali hua tete sometimes, wewe unayetoa msaada kesho na kesho kutwa utakuja fikwa na jambo hao hao wanaokuomba ndio watakaokusaidia hivo saidia pale inapobidi na iwe ni siri ya moyo wako na uliyemsaidia pamoja na Mungu wako.
 
Sawa mkuu
Ila tatzo wanajiona wnyw ndo wanajua kuatafuta kwa vle wana familia mm sina kama sina akili za kimaisha
 
Sawa mkuu
Ila tatzo wanajiona wnyw ndo wanajua kuatafuta kwa vle wana familia mm sina kama sina akili za kimaisha
ukipata mke au mume sahihi umepata tulizo la nafsi, ukiweza kuridhika na hali uliyonayo huku una mtu ambae unaona kabisa tunaendana nafsi yako hua na amani, wewe hilo lisikuchanganye, omba tu upate mtu sahihi ndio utaelewa kwan ndoa ni zaidi ya kutafta riziki pekee
 
Maisha ya ndoa yanahitaji:

Akili,
Uvumilivu,,
Kusikilizana,
Kuheshimiana na
Kusameheana,

Ndoa nyingi huingia matatizoni pale mmoja wao anapojiona ni bora kuliko mwingine,au pale mmoja wao anapojiona ana haki zaidi kuliko mwingine,

Ndoa ni maelewano na mapatano,siku zote jaribu kumtanguliza mbele Mungu,siri zenu za ndani ziwe zinaishia kwenu tu wala mmoja wenu asijaribu kuzitoa nje hadharani,huko nje kuna watu wanasubiri mkwaruzane tu ili nao waingilie kati na kucheza na akili zenu,

Ndoa ni heshima na ndoa hujenga familia bora iliyobarikiwa na mwenyezi Mungu,kwani Mungu amehimiza ndoa na kukataza zinaa.
 
Sawa mkuu
Ila tatzo wanajiona wnyw ndo wanajua kuatafuta kwa vle wana familia mm sina kama sina akili za kimaisha
Live ur life,acha kuangalia watu wala kusikiliza watu.ulikuja duniani peke yako na utaondoka peke yako,ishi maisha yako na usiishi maisha ya kumfurahisha mtu,

Good luck.
 
Hakuna mahusiano kati yakuomba msaada na ndoa wengi wanaoomba msaada hawana wake hapo vipi? Ila ulitumia kauri mbovu sana yaani mtu anakuomba msaada alafu unamwambia habari zakumlishia familia yake! Aaa mtake radhi ndugu.fanya haraka uoe isije ukaolewa wewe baada kakufumaniwa
 
Pale mvaa viatu anapojaribu kumvalisha viatu asiyetaka kuvaa viatu.:D:D
 
Wachane tuu ukweli ndio huo wameoaa alafu kuhudumia familia shida sasa ulioa ya nini baki single tuu kama huna mihela

Nani alikudanganya eti mwanamke anakupenda wewe mwanaume...mwanamke anafuata ulichonacho. Mwanawane usiwasaidie kabisa kila mtu abebe mzigo wake....wameoa basi wawetagari kuhudumia familia zao wala usiwasaidie mbona wao hawakusaidi kwa kukupa wake zao ugegede ukiwa na ukame.
 
Ishi maisha yako usiangalie Binadamu wa dunia hii wanaongea nini au wanafanya nini juu ya maisha yako.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom