mjizu123
JF-Expert Member
- Mar 19, 2016
- 349
- 370
MAISHA YA MWANADAMU NI HATMA
Ulishawahi kujiuliza kwamba Maisha yetu yote ni hatma iliyopangwa au tunaishi kwa muongozo wa akili zetu kwa kufuata kanuni za maisha yetu.
Ni kawaida sana kwa watu wengi kusema kuwa kila kitu maishani kimepangwa na kila mwanadamu ataishi kwa mipango yake kwa kadri vile alivyopangiwa ila bado kwa kutumia hoja hii aina ya watu hawa huja kupingana nayo katika mambo mengine.
Kama kila kitu duniani kimepangwa basi hata ulimwengu umepangwa na unajiendesha kwa kadri ya mipango yake na maamrisho yake yote na ndio maana nyota huzaliwa kila baada ya muda na ndio maana hutanuka kwa nguvu ya ajabu na ndio maana kila sayari zipo katika mwendo wake na Mvua zinanyesha kila baada ya wingu zito kutanda angani na baadae kuyeyuka na kuanguka kama mvua.
Je, unakubaliana na Usemi huu?