Maisha ya Mlimwengu Boarding School:4

Maisha ya Mlimwengu Boarding School:4

Mohamed Ismail

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2014
Posts
227
Reaction score
246
Wakati wa kurudi rafiki yangu mmoja aliniambia kuna kitu inabidi tukitumie....nikamuuliza nini akanionyesha bangi mguuni kwake iliyokuwa kwenye soksi. Alivyonionyesha nilishtuka sana lakini sikutaka kuonyesha machoni kwake kuwa nimeshtuka. Nikawa najiuliza maswali mengi kichwani mwangu ambayo sipati majibu yake. Kwanza nikakumbuka nyumbani baba aliwahi kuniambia kuwa nikivuta bangi nakuwa kichaa, na kitu kingine wanaovuta bangi huwa wanaonekana hawana akili kichwani mwao. Wakati natafakuri mapigo yangu ya moyo yanaenda mbio. Nikajiuliza tena mbona siku zote huwa tuko pamoja au ndio anaanza kujifunza kuvuta na kama alikuwa anavuta mbona hana dalili za watu tuliowazoea kama wavuta bangi...na kama anavuta atawezaje kuwa rafiki yangu wakati nyumbani walishanipa ushauri wa kuepuka makundi ya watu wenye tabia mbaya....hawa si ndio inabidi niwaepuke na mbona ni rafiki yangu kitambo. Wakati najiuliza hayo maswali sikupoteza muda mwingi sana. Nilimuambia kuwa aisee mimi siwezi kutumia kwa sababu mimi mwenyewe bangi nikiongezea bangi nitavuruga. Nikamuambia angalia washikaji wengine wanaweza kutumia. Alikubaliana na mimi lakini ilikuwa kinyonge maana aliniaminia kama rafiki yake ndio maana akanishirikisha. Na hii kitu wanafunzi wengi waliambulia kuvuta kwa kutaka kuwaprove watu kuwa ni wajanja kwa kujaribu kila kitu kinachotokea mbele yao. Ndio maana wanafunzi wengi wanajiingiza kwenye utumiaji wa madawa ya kulevya kwa ujuaji mwingi. Mlimwengu mimi nilikuwa sipo tayari kuonekana mjanja kwa jambo ambalo sijakubaliana nao. Na hii ilinisaidia wakanielewa waliokuwa wanatumia na urafiki wetu ukaendelea ukifika muda wa kuvuta walikuwa wanatukwepa ambao hatuvuti ila baadae wengi walinizoea wakawa wana uwezo wa kuvuta hata nikiwepo. Na mara nyingi ilikuwa ni usiku au jioni wanakwenda mnarani au Mombasa. Kuna kipindi nilikuwa najiuliza maswali je ikitokea polisi wakaja au walimu na mimi ningekamatwa kama mvuta bangi maana hakuna ambaye angenielewa kama mimi siyo mvutaji. Mimi siku zote niliamini kuwa kutatua tatizo siyo kulikimbia bali ni kupambana nalo ndio maana sikuwahi kuachana nao ingawa baadhi ya maamuzi yao nikiona sijayaafiki nilikuwa sishiriki. Katika makundi ya wavuta bangi kuna watu iliwafanya wawe wagomvi, wengine wakivuta wanakuwa wapole, wengine wanakuwa wachafu wengine inawapelekea kuwa kinyume kabisa na utaratibu wa shule....na baadhi waliamini bila kuvuta hawawezi kuelewa darasani. Yote hiyo mlimwengu mimi nilikuwa nayaona nikiwa nje ya darasa. Wengine tulikuwa tulikuwa hatufuati sheria tu kwa ajili ya puberty stage (balahe). Kumbuka shule yetu ni wavulana tu basi watu ndio balehe zinatutuma kuanza kutongoza wasichana. Kwa kipindi hicho mabeki tatu wa walimu walipata shida sana na watoto wa walimu. Shule yetu ilikuwa karibu na shule ya msingi wengine walithubutu kwenda kuwatongoza wanafunzi wa darasa la tano hadi la saba maana na wao walikuwa walishavunja ungo. Wengine walijifariji kwa kuandikiana barua na wanafunzi ambao wametoka eneo moja halafu awe anasoma Bwiru girls au Nganza. Lakini mara nyingi ilikuwa Bwiru girls almaarufu umendeni. Wasichana wa Bwiru girls tulikuwa tunawaita mende. Ukishakuwa na rafiki yako yuko Bwiru girls basi utatudanganya kuwa ni mpenzi wako au akiwa rafiki yako alikuwa anakusaidia kupata demu kwa kukupigia pasi ya kisigino na kuchukua mrembo kiurahisi. Na ambao walikuwa na ndugu zao umendeni ilikuwa rahisi kupata mpenzi. Mambo ya connection hayajaanza leo bana ndio maana sasahivi hadi msibani kula mpaka uwe na connection. Hii ndio asilia yetu. Kumbuka hapo mlimwengu mimi nililkuwa ni mjanja mjanja ila domozege. Mimi kwa kipindi hicho sikuwa mpango na mambo ya wasichana ila nilikuwa nawasindikiza rafiki wangu wanapoenda kutongoza. Sisi ndio wale mashabiki ukitongoza ukatoswa nitakucheka wiki nzima na kukutania. Basi wengine wakawa wananikwepa ili nisijue akishakubaliwa ndio anakuja kunitambia. Mambo ya kushawishiana bana wakaanza kusema mimi ni domozege ikawa tukienda sehemu wananiitia msichana halafu wananikimbia ili niadhirike. Basi na mimi kwa akili yangu nikiitiwa msichana. Akishakuja mbele yangu...naanza kumuambia sikiliza hawa hawana lolote wanakupenda wao ila wanakuogopa na mimi ndio huwa wananitegemea ndio washakuelewa hivyo. Hao wasichana wanaamua kuondoka basi kutokana na majibu yangu wakaacha hiyo tabia ya kunisakizia.
Na mtu ilikuwa akiandikiwa barua basi ataonyesha darasa zima na enzi hizo barua nyingi zilitumwa kwa njia ya posta. Karatasi zilizotumika ni zile zenye makopa makopa ya love na maua na barua inapuliziwa perfume. Na chini unakuta umewekewa dedication song za westlife my love na nyimbo nyingine za malavidavi. Achana na mambo ya wadada wa siku hizi mesaage zao za whatsapp ni za mkato. Mapenzi yalikuwa zamani mtu akiisoma ile barua anajisiikia kama yuko peponi.
Na shida tuliokuwa nayo moja tukiwa parade akipita mdada njiani wanafunzi wote wanageuka hata kama mwalimu alikuwa anazungumza. Walijitahidi sana kutuwekea mafuta ya taa kwenye chakula. Hadi leo huwa najiuliza aliefanya utafiti wa mafuta ya taa mbona huwa hapewi heshima yake na sijui nani alianzisha kwenye shule za boarding. Kuna wakati maisha ya sasahivi unavurugwa na mahusiano unataka utumie mafuta ya taa...
Na uzuri wa shule zetu kila mtu alikuwa ana shati lake zuri na kiatu kwa ajili ya mtoko. Na mavazi hayo yalivaliwa siku za debate au kwenye shughuli inayotukutanisha na shule za jinsia tofauti. Lakini tukiwa wenyewe watu wanavaa shati leupe hadi unashindwa kutambua ni rangi gani na wenzangu na mimi kumaliza wiki mbili bila kuoga ilikuwa kawaida. Aisee boys tulikuwa wachafu na ukijikuta una uchafu wa asili kama mimi ukaongezea na uboys ndio kabisaa. Kipindi hicho uvaaji wa boxer ilikuwa bado wengi wao walikuwa hata chupi hawavai. Akivaa suruali anaenda darasani na mkanda hamna wakati mwingine tako liko nje. Na wengine walikuwa lazima wapate chawa na tulikuwa tunawaita faiba. Chawa wana kiherehere sana unakuta mtu kavaa shati lake jeupe ila jua likiwaka chawa anachomoza lazima akuaibishe. Ndugu yangu mmoja sasahivi ni mchungaji ila faiba walimsumbua sana. Maisha ya boys ilikuwa mtihani ukitaka kukata gogo lazima uvue nguo zetu maana bila hivyo utanuka mwili mzima harufu ya choo. Wenzangu na mimi tulikuwa tunakata gogo porini.. sijui hizi kampeni za nyumba ni choo zinafika mashuleni.Tulikuwa tunakata gogo kwa kuhamahama ndio maana uoto pale ulistawi vizuri tulijitahidi kuweka mbolea. Ila huwa najiuliza kipindi kile U.T.I ilikuwa wapi?. Maana ingekuwa kipindi cha sasa wengi tungedhuriwa na U.T.I. Tulikuwa tunakata gogo porini halafu ziwani ndio unaenda kujisafisha kuna watu walikuwa akili za kitoto unakuta mnaoga ziwani mara unaona gogo linaelea juu ya maji. Mkishaliona mnatoka ndani ya maji appetite ya kuogelea inaisha.
Shuleni tulijifunza sana ushirikiano kwa kutumia vitu pamoja na kushirikiana unapoishiwa pocket money. Ingawa tabia ni ngozi wengine chao kilikuwa chao ila cha kwako ndio anataka mtumie wote kwenye maisha watu wa hivyo hawakosekani.
Maisha ya Mlimwengu yaliendelea na shule nikazidi kuizoea na sisi ambao tulikuwa tuna ndugu Mwanza ilikuwa lazima weekend uende kuwatembelea ubadilishe diet kidogo. Sasa ilikuwa ukifungiwa chakula ukaja nacho...watu walikuwa wanakufuata kila sehemu unayoenda kumbe shida yao mpaka mle chakula wakishakula wanasepa. Kweli mwenye nacho lazima anyenyekewe.
Kuna wengine walikuwa wakiishiwa pocket money wanaanza kusali akipata hela anaacha. Ndio nikaamini ule msemo wa pata hela tujue tabia yako.
Mara nyingi ukiwa form one ilikuwa lazima uwe na master wako ambaye ni kama kaka yako anakuwa anakuangalia na kukuelekeza mambo ambayo huyajui. Mlimwengu mimi sikuwahi kuwa na master. Ila nilikuwa nalala na Seleman yeye alikuwa form 4 na bweni langu la kawawa nilikuwa na watu kama George, Erasmus, Ndulila, Zema , Revocatus (Manyusi) walikuwa wananichukulia kama mdogo wao hivyo nisingeweza kusumbuliwa na mtu na nilikuwa dogo janja. Na kingine mikono mitupu hailambwi nilikuwa kati ya watu ambao sikosi nyuka(sukari) kwenye stock yangu kwa wale wapenzi wa chai tulikuwa tunajuana. Ila nilikuwa najiongoza nakumbuka nafanya yote bado darasani nilikuwa gud. Ikifika mwezi wa ramadhani waislamu ndio mnajuana...maana tulikuwa tunapewa msaada na waislamu hivyo chakula kilikuwa kizuri. Basi muda wa futari wanafunzi wote hata wa dini tofauti wanatamani wawe waislamu. Mkiwa msikitini unakuta nje wamekusubiri ili uwape wali na sasa unachagua umpe yupi umuache yupi. Kuna watu hadi daku wanaamka nao ili mule nao mara nyingi nilikuwa sili daku naamka kwa ajili yao nawachukulia chakula.
Hayo ndio maisha ya boarding kipindi cha mahindi yalikuwa yanaibwa mahindi kwenye mashamba ya shule na ya walimu na kwenda kuchomwa porini. Kuna disko lilifanyika awamu nyingine na hiyo tulikuwa tumewaalika Mende. Na ilikuwa migongano mikali kati ya wanachama wa disko tualike shule gani. Sisi tuliowengi tulipiga kura waje Mende. Kwanza Nganza walikuwa wanakuja wengi ni Advance na kipindi chetu hawakuwepo form one ndio walikuwa wameacha kupokea form one. Hivyo tukaona mende ndio size yetu wale wakubwa ingawa ilizoeleka Nganza walipendwa na Bwiru Boys na Mende walipendwa zaidi na Nsumba. Basi sisi form one yetu waingia disko walikuwa wengi hivyo kura zikawa nyingi na mende wakaja. Basi kama kawaida tukajiandaa nakumbuka hapo nilikuwa nimevaa ribbon kichwani kama Nelly na nimepiga full white kiukweli nilipendeza. Kilichotokea Mende walikuja kama Ishirini basi tulikuwa wavulana wengi na wasichana wachache. Disko lilivyoanza walikuwa wanaringa sana. Kuna wadada walikuwa wanaudhi anakuja disko la wavulana halafu wanataka wacheze wao kwa wao...ukimfuata anaenda kuegemea ukuta wenye akili kama zangu nilitamani hata ukutani tupake uchafu. Watu wengi disko lile walicheza kavu hawakupata mtu wa kucheza nao. Mlimwengu mimi nilikuwa nilishakuwa mjanja nilicheza nao wengi sana na walikuwa size yetu kabisa. Basi kuna dada mmoja yeye alikuwa form 3 basi nilicheza naye sana ila story nilikuwa sina tukiwa tunacheza muziki nabaki narudiarudia nyimbo kwa kuuma maneno ili nionekane na mimi nimo. Hata akipumzika nilikuwa namsubiri tunacheza wote. Hata nikimkuta na mtu namchukua kama msichana wangu. Kumbuka hapo hata jina lake sijamuuliza. Natamani nitongoze lakini moyo unagoma kwa uoga. Ili na mimi nianze kutamba kama nina demu. Basi muziki ulivyokuwa unakaribia kuisha wanaweka nyimbo za blues( zero distance) basi hapo waswahili wanasema mizuka kama yote na minara yote inasoma mtandao labda uwe hanithi siyo kwa kukumbatiana huko. Ila hapo hata jina lake sijamuuliza na maongezi yetu ni kwamba ananiambia nimechoka na mimi namuambia pole. Ila hapo najiapiza moyoni lazima nitongoze na nilikuwa nikiona rafiki zangu wananiangalia na mimi nilikuwa namshika kwa masifa...na waliokuwa wanachungulia dirishani niliwapa taabu sana. Mara paap nilimuona kiongozi mmoja wa dini yetu akija kuchungulia kuangalia tuliohudhuria basi na mimi nikawa namuonyeshea nilivyo mahiri kushika kiuno. Basi mpinzani wangu mmoja Andrew alivyoona nimekamatia mtoto akajua tayari nimepata demu basi naye hapohapo akafanya mpango ili apate demu ila angejua maskini yangu mimi domo zito. Gahutu yeye alikuwa hana mpango ni watu ambao ni makatuni hata style zake ni za kuchekesha. Hapo Edgar Benja wote walikuwa wamekamatia watoto. Mara paap muziki wa mwisho ukapigwa sijasema lolote na muziki ukazimwa. Basi muda wa kutoka Mende walikuwa wanarudi shuleni kwao kwa kutembea kwa miguu kwa sababu shule yao ni karibu na kwetu. Muda wa kutoka kila mtu anatoka kamshika mkono au kiunoni mlimbwende ili mradi kuwaumiza wale wanaochungulia. Basi na mimi nikafanya hivyo wala nikimshika alikuwa hautoi hata mkono lakini sina ujanja wa kuendelea. Ndugu yangu Edger akaninongoneza ebu fanya mambo nikamuambia tayari kwa ishara basi yule mlimbwende kasimama. Na kiukweli Mwenyezimungu mkubwa yule mtoto alikuwa kajaliwa yuko natural na umbo la kiafrika ngozi laini utadhani haogi maji ya ziwani anaoga maji ya Dasani. Tulitembea hatua kama kumi nikajipiga moyo konde nikamsimamisha...akasimama....huku kaniangalia usoni.....
Je mlimwengu ninaenda kumuambia nini? Na nini kilitokea?
Tukiwa tunaenda kutimiza miaka 100 tangu Bwiru Boys ianzishwe. Nitakuwa naeleza matukio niliokutana nayo.
Episode 4
Stay tuned
#mlimwengumimi
#BwiruboysAlumni
#100yearsAnniversary
FB_IMG_1549728287814.jpeg
 
Stori nzuri sana leta episode nyingine mwamba wa bwiru boys
 
Aisee mkuu nimefirah sana story yako....mm nmesoma njombe boys(Njoss) hakika umerudisha far back nmecheka baadhi ya vipengele aiasee....hasahasa suala la uchafu...mf; mm nilikuwa siogi kwa siku 6 yaan jumatatu had jumomos ikifika jumapil naoga ndoo 6 kwa pamoja et nafidia kila ndoo na siku yake....
 
Back
Top Bottom