Maisha ya kisiasa.

ADRIAN

Senior Member
Joined
Dec 31, 2012
Posts
113
Reaction score
27
Maisha na Siasa Siasa ni maisha. Magari tunayotembelea ni siasa, nyumba unayolala ni siasa, shule unayosoma ni siasa, chakula unachokula ni siasa, maji unayooga ni siasa, dawa unazozipata hospitalini ni siasa, nguo unazovaa ni siasa, vocha za simu na simu unazonunua ni siasa.

Ila ccm imebadili siasa kuwa chafu. Sasa chadema tunataka tuifanye siasa kuwa maisha na kuwa siasa safi. Kwa muda mrefu watanzania tumekuwa tukiambiwa kuwa siasa ni mchezo mchafu kutoka kwa viongozi wetu waliotutangulia ambao wangetuhimiza kuipenda siasa badala ya kutukatisha tamaa. Lakini ninachoweza kusema ni kwamba, walitumia kauli hizo ili wapate nafasi na mwanya wa kutunyonya, walitumia kauli hizi ili waweze kuficha kodi zetu kwenye mabenki ya nje ya nchi, walitumia kauli hizi ili waweze kusalia madarakani milele, walitumia kauli hizi ili waendelee kuuza madini yetu kwa wageni, walitumia kauli hizi ili waendelee kujipatia ardhi kubwa kutoka kwa wananchi wa kawaida, walitumia kauli hizi ili waweze kuuza kwa urahisi pembe za ndivu kama watawala.

Kutokana na ukweli halisi kwamba siasa haijawahi kuwa mchezo mchafu, nawaasa, nawashauri vijana wenzangu, wazazi wangu, dada na kaka zangu kuipinga kauli ya kuwa siasa ni mchezo mchafu bali tusimame hadharani na kuisafisha siasa na kuiona kuwa ni mchezi mzuri ambao hujenga

1. hujenga urafi,
2. huimarisha afya,
3. huinua vipato vya wachezaji na mashabiki,
4, hutengeneza umoja na mshikamano,
5. huondoa tofauti za kidini na kikabila nk.

Falsafa ya Siasa (Political Philosophy) inasema kuwa politics is concerned with economics and organisation of Society. Hivyo, tukiiheshimu siasa tutakuwa tumeheshimu uchumi na ustawi wa jamii yetu kwa ujumla lakini ikiwa tutaibeza siasa, tutakuwa tumebeza uchumi wetu, jamii yetu na kwa mantiki hiyo, tutakuwa tumejenga msingi mbaya wa uchumi na jamii.

Watanzania tuungane na Chadema katika kuweka sawa/sahihi kauli iliyoasisiwa katika taifa letu na viongozi wa ccm ambao ndo wananufaika zaidi na kauli hii kwa kutunyonya kupita kiasi. Na Mutta Anselimi Adrian (mwl) katibu mwenezi Chadema Singida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…