tutafikatu
JF-Expert Member
- Dec 17, 2011
- 3,327
- 4,624
Gari ya ulanzi imepita mbele yangu, nikakumbuka mbali sana.
Mimi ni mtoto wa 'bush'. Nimebahatika kuishi miaka mitano kijijini uswekeni. Niliishi Njombe, ndaani kabisa huko, wanaita Palangawanu. Tulikuwa tukitembea kwa mguu toka Ilembula hospitali hadi Palangawanu (nadhani km 15 hadi 20, sikumbuki, nilikuwa mdogo sana). Mzazi wangu mmoja alikuwa mwalimu huko (si wenyeji). Basi tulikuwa kama miungu wadogo, hata ukicheza mpira wanaogopa kukukanyaga, "mtoto wa mwalimu huyo".
Nikiwa mtoto mdogo wa miaka sita hadi tisa, mzazi alikuwa na tabia ya kunituma kuchukua ulanzi na maziwa, kwa wana vijiji walioko mbali. Ni mazingira mazuri, ya kushuka mabonde, kuvuka mito, na kupanda vijilima. Njiani kumejaa mianzi inayogemwa. Kuna 'masasati', kuna 'vitowo', kuna miwa, kuna embe, kuna 'makusu' sijui. Yaani ilikuwa kwangu neema, sijui umaskini wala utajiri. Kwangu yale yalikuwa maisha. Wahindi wanasema "'fullu' life, no tension".
Ilikuwa kawaida kwa watoto kunywa ulanzi unaogemwa njiani na hata kunywa ule uliotumwa kuuchukua. Siku moja nimefika nyumbani hoooooi, nimekunywa ulanzi mtogwa mpaka nimelewa. Bahati mbaya, nusu ya lita tano ya maziwa iliishia tumboni. Nafika nyumbani napepesuka, badala ya kupata kichapo, mzazi akaishia kucheeeeka tu kwa vituko vya mlevi mtoto.
Ingawa sinywi tena pombe, na sidandii magari barabarani, lakini hizo ni baadhi ya siku nilizozifurahia maishani.
Umeishi kijijini? Unakumbuka nini?