Maisha ni kupeana support

Maisha ni kupeana support

Natafuta Ajira

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2020
Posts
12,199
Reaction score
33,734
Siku moja nikiwa katika kibarua cha kuwasaidia mafundi ujenzi kazi ndogo ndogo mfano kuchanganya cement na mchanga, kuchota maji, kusogeza tofali n.k (hata kama hatuna kazi ya proffesional tulizosomea chuo ila tusibwete tu bila kujishughulisha na chochote)

Sasa wakati fulani napata msosi ili niweze kuendelea na kazi alipita kijana mmoja wa mauzo ya mahitaji ya nyumbani akiwa amebeba bidhaa zake dawa za meno, mafuta, losheni, sabuni n.k kama kawaida akaanza kuzinadi bidhaa zake kwangu nikamsikiliza kwa makini na nikauliza maswali kadhaa (sio maswali ya kutaka kumzodoa au kuonekana mimi najua sana) nikanunua bidhaa moja ilikua sabuni ya kuogea na mwisho kabisa nikampa mawazo yangu pale ambapo naona anaweza kujiboresha katika harakati zake za mauzo maana mimi nishawahi kuwa mtu wa mauzo pia katika benki moja hv kubwa kwa hapa Tanzania kwaiyo ninazo A.B.C za mambo ya sales and marketing ingawa sikumwambia kama na mimi nishawahi kufanya kazi inayofanana na yake

Kusema kweli kwa siku iyo sikua na uhitaji wa bidhaa anazouza na uyo jamaa hata sikua najuana nae lakini iyo elfu moja yangu mfukoni nikasema ngoja nigawane na jamaa kusapoti harakati zake na ku'share maarifa ya kile ninachokijua kuhusu biashara anayofanya jamaa

Funzo kwetu wote, tupeane support katika harakati zetu, msaada sio lazima connection ya kazi au kununua bidhaa za thamani kubwa wewe support tu chochote ambacho kipo ndani ya uwezo wako hata kama sio kikubwa angalao inaleta hamasa kwa mtu unaempa support kuendelea kutafuta zaidi

Especially sisi job seekers sio kwa sababu tunatafuta ajira basi tujione sisi ni watu wa kupewa support tu hatupaswi kutoa support kwa lolote, pale ambapo tunaweza ku'support movements za wenzetu tufanye ivyo hata kama ni kidogo
 
Nakufuatilia!

Hii ni mada yako ya pili nakutana nayo,unaandika vitu sensitive sana ambavyo vipo kwenye jamii tunayoishi.wazee wanasema ukinunua kitu kwa mchuuzi humchangii akajenge ghorofa au kununua gari ila umemuwezesha na yeye aione kesho yake.
 
Ni kweli mkuu pamoja na watu kulilia connection ila ukweli ni kwamba wapo wengi tu wanapata izo connection na hawazitumii vizuri mwishoe wanarudi tena kule kule chini walipotoka
au wengine wanachukulia poa tu hawawi serious
 
Back
Top Bottom