pet geo pet
JF-Expert Member
- Jun 30, 2018
- 518
- 815
Wakuu habari za muda huu!
Tukiwa tunapokea matokeo kutoka sehemu mbalimbali ya Tanzania, ikionyesha CCM inashinda kila mahali kwa kura nyingi sana.
Mimi ni kijana nilizaliwa(1995) nilikuta mfumo wa vyama vingi vya siasa, katika somo ya Civics nimesoma kitu kimoja kinaitwa check and balance. Natafakari hapa maisha ya chama kimoja yatakuwaje.
Sina hakika kama kutakuwa na mbunge wa CCM anaweza kuikosoa serilikali yake kwa utawala huu.
Ubeze usibeze upinzani una umuhimu wake katika kujenga taifa hasa katika kuibua maovu yanayofanywa na serilikali.
Naombeni mloishi miaka ya nyuma kidogo maisha ya chama kimoja yapoje nijiandae kuyapokea.
Cheki huyu Taira...anavyo jitairisha humu ndani.Wauliza baba zako walioishi before and after vyama vingi watakuambia.
Nitajie maadui watatu wa taifa la Tanzania.Walioaribu ni wapinzani wenyewe kwenye mambo mengi sana,mfano:.
a) kupinga na kubeza kila jambo zuri la mandeleo.
b)Covid-19 ni pigo moja baya sana kwa wapinzani kubeza msimamo wa JPM.
c)kuonyesha dhahiri kwamba wao wanawategemea zaidi watu kutoka nje kuliko watanzania,yani jambo dogo tu eti "Armstadam kasema" mara "Armstadam kamuandikia barua Rais Magufuli"
Sasa kwa hali iyo ni bora watanzania tuongozwe na chama cha CCM mpaka utakapo patikana upinzani wenye vyama vyenye kujielewa vitakavyo shiriki kwa dhati kwenye kuijenga nchi na si kususasusa Bungeni na kubeza kila jambo la maendeleo.
maadui watatu wa taifa la Tanzania.Nitajie maadui watatu wa taifa la Tanzania.
1.
2.
3.