Maisha bora ni nini? Tuyapateje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maisha bora ni nini? Tuyapateje?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Shoo Gap, Jun 11, 2010.

 1. Shoo Gap

  Shoo Gap JF-Expert Member

  #1
  Jun 11, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 236
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Niliipitia makala ya Privatus Karugendo katika Gazeti la Raia Mwema Toleo Na 136 la tarehe 2 - 9 June yenye kichwa "Hii ndiyo ilani ya Wazalendo 2010". Ingawa nina mpango wakukitafuta kitabu cha Dkt. Godfrey B.R. Swai kinachoitwa: Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2010: Mustakabali Mpya wa Maisha Bora na Mwisho wa Viongozi Waporaji na Wabadhirifu ili kujifunza kupitia mchango wake wa mawazo ambao kwa hints alizoonesha Privatus kinapaswa kusomwa na kila Mtanzania.

  Maisha bora kwa kila mtanzania ilikuwa kauli mbiu ya CCM katika uchaguzi wa 2005, ingawa kila chama kina mawazo haya haya ya kuleta maisha bora kwa kila Mtazania. Tatizo kubwa limekuwa ni namna gani SERA za hivi vyama ni BORA kutufikisha hapa. Lakini tunapaswa kujiuliza pia Sera bora ni zipi?

  Mambo mengine ya Msingi aliyoyataja ya kutufikisha kwenye maisha bora ni:-

  Katiba bora
  Uchaguzi bora
  Utawala bora
  Mipango bora

  Vyote hivi vinapaswa kutolewa maana yakinifu.

  Ukiibuka na kusema tu utaleta maisha bora bila kuwa na tume bora na huru ya uchaguzi ni uongo mtupu na ni kudanganyana tu. Nadhani tulipaswa kuchagua viongozi na watendaji bora na huru wa tume uchaguzi kabla ya kupiga kura za madiwani, wabunge na Rais. Lakini tukiendelea kuwa na viongozi wa tume wanaoteuliwa na Mwenyekiti wa chama kimojawapo huu ni usanii mkubwa.

  Haya yote hayatawezekana tusipokuwa na katiba bora na huru inayoelekeza haya yote. Katiba bora na uchaguzi bora utatupa viongozi bora waliotayari kusimamia sera bora, kwa mantiki hiyo kuwa na utawala bora wenye mipango bora itakayosimamia maslahi ya watanzania wote kwa usawa na haki.

  Naomba wote tutafute kitabu hiki ili tufahamu wapi tuanze, kufikia maisha bora.
   
Loading...