Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,745
Nipo radhi Magufuli kuongezewa hata miaka selasini kama atatufikisha kwenye maisha bora kwa kila Mtz.
Tulinganishe nchi mbili zenye utawala wa kifalme na nchi yetu ya Tanzania,Kisha utatafakari kati ya nchi hizo za kifalme na nchi yetu tunayobadilisha mafisadi kila baada ya miaka kumi na kuweka fisadi mwengine. Yetu ama za kwao ndio ziko katika mustakbali mzuri?
Utafiti uliofanywa na Maktoob Research (asasi ya utafiti kupitia internet katika nchi za Mashariki ya Kati na Afrika Magharibi), machi 2008, imeiweka Oman kuwa ndio taifa la kwanza lenye raia wenye kufurahia maisha ikifuatiwa na Saudi Arabia, miongoni mwa mataifa ya Ghuba,mataifa ya Afrika Kaskazini, na mataifa ya mashariki mwa bahari ya Mediterranean.
Kwa sasa Oman, elimu na huduma za afya ni bure, watu hawalipi kodi ya mapato, maisha ya raia ni mazuri, utajiri wa Oman umewanuifaisha wanafunzi wa KiTanzania pia, kwani kwa mwaka wa tatu mfululizo, imeanza kutekeleza mpango wake wa kufadhili vijana wa KiTanzania kwa masomo ya juu.
Hadi mwaka 2000 kipato cha mu-Oman mmoja mmoja kilikuwa kwa mwaka ni Dola 10,000 za Marekani. Kwa lugha rahisi hali ya kiuchumi ay Oman inayoongozwa kifalme,ni nzuri zaidi.
Hata ripoti ya UN Sustainable Development Solutions Network (SDSN), mwaka 2013 Oman ilikuwepo katika orodha ya mataifa ambayo watu wake wanaishi kwa furaha.
Oman na Saudia Arabia ni mataifa yanayoongozwa na tawala za Kifalme.
Suali la kujiuliza ni kwamba kuna ripoti yoyote duniani ilishawahi kusema, “Watanzania ni raia wenye furaha na maisha?
Zipo ripoti nyingi zinazotaja nchi zenye furaha, kisha kwa kupunguza kazi ripoti husema, “nchi zisizo na furaha kwa Afrika ni zote zilizo kusini mwa jangwa la Sahara” .Tanzania imo kundi hilo.
Nirudie kusema kuwa , aina ya utawala si tatizo kwangu, kama ni mfalme na Malkia, wakati hakuna haki ya binaadamu inayovunjwa na raia wamenawirika kutokana na uongozi huo.
Au uongozi wa kubadilisha viongozi kila baaada ya miaka kadhaa kwangu sio tatizo, pia kama ni kiongozi wa muda mrefu ambaye ameinawirisha nchi na kuondoa umasikini na matatizo mengine mengi kwangu hali kadhalika sioni tatizo la utawala huo.
Ila tatizo hujitokeza linapokuja suala la,“utawala unatawala kwa namna gani”. Mfalme ataiyongoza nchi katika mafanikio au mafunikio? Rais atatupeleka katika maendeleo au utumwa mambo leo? Ni utawala wa mkono wa chuma au mkono wa huruma?
Magufuli akitufikisha huko kwenye maisha ya wanaofurahi na kupewa daraja katika ngazi za kimataifa basi nitakuwa radhi hata akiongeza miaka mingine selasini.