Uchaguzi 2020 Maisha baada ya uchaguzi: Je, zoezi la Uchaguzi linajitosheleza kwa Wananchi kwenye suala zima la Demokrasia?

DaudiAiko

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
302
274
Wana bodi,

Ni jambo la kushukuru kwamba tumeweza kupiga kura salama na kuendelea kupokea matokeo kwa utulivu. Vilevile ni vyema kuona kwamba wana siasa kwa kiasi ki kubwa, wameweza kuheshimu maoni ya Watanzania kwa ujumla. Mengi yamejadiliwa kuhusu mapungufu ya uchaguzi huu ikiwemo kutokuwepo kwa tume huru ya uchaguzi na kutokuwepo kwa katiba mpya. Hayo yanaweza kuonekana kuwa mapungufu yenye uzito lakini kuna mengine ambayo ningependa kueleza.

Ninachokipa kipaumbele ni jinsi gani zoezi hili la kidemokrasia halijitoshelezi kukidhi mahitaji ya wananchi. Mtanzania yeyote anafahamu kwamba kuna uchaguzi kila baada ya miaka mitano na kwa yeye kura yake MOJA TU ndio njia pekee kuweza ku wasilisha dukuduku lake au kupongeza maendeleo yake. Maelezo haya yanaashiria kwamba mwananchi yeyote anachangia kwa kiasi kidogo sana kwenye uendeshaji na maendeleo ya nchi yake.

Unaweza kukanusha kauli yangu kwa kusema kwamba Mbunge, Diwani au Rais ni muwakilishi ambaye anatosha kufanya kazi yake lakini hata kwa ngazi ya jimbo, kazi za uendeshaji na maendeleo zinafanywa kwa usiri sana bila kuwahusisha wananchi.

Njia moja na muhimu sana kutatua tatizo hili ni kuhakikisha kwamba viongozi wote haswa wabunge wanajituma na kufanya shughuli zao kwa umakini sana.

Vile vile serikali ingeweza kufikiria kuchukua maoni mbalimbali kutoka kwa wananchi kwa njia ya kura za maoni au kupata "Feedback" kutoka kwa wananchi kwa njia hiyohiyo. Hili linaweza kuleta manufaa makubwa kwa wananchi likifikiriwa kwenye katiba mpya.

Tafakari,

Jummah Kareem.
 
Back
Top Bottom