Grealish10
Senior Member
- Mar 25, 2020
- 104
- 295
thats nature binadam lazma afariki bila kujali umri wake,
hilo ni jambo tuu ambalo lingetokea na kukuumiza tuu hata baada ya miaka mingi mbele..
kufa niwajibu na lazma tujiandae tuu kuwa wapendwa wetu iko siku tutawakosa.
mimi nilifiwa mfululizo mwaka jana lakini nikakumbuka tuu kuwa binadam sisi ni wapitaji tuu.
usiwaze kujiua sababu utakuwa umetengeneza tatizo kubwa zaidi kuliko unavyodhani.
jikaze jaribu kutoka nje mbali na mazingira kumbukishi ya mwanao.
safiri kidogo km uwezo upo.
jichanganye na ndugu jamaa au marafiki..
piga mastori sana cheki muvi.
basi muda ukifika utapona tuu uwe sawa
Acha kufa akiugua tuu moja haikai wala mbili..Maneno mengine ni ya kufarijiana tu ila kuzika mtoto kusikie tu.
Hakuna huzuni kubwa kama kwa baba kumzika mwanae.
Kaka naomba nisaidie mistari ya ayubu katika bibliaPole mkuu, mtangulize Mungu! Kama unasoma biblia kumbuka Ayubu alipoteza kila kitu lakini hakumwacha Mungu
Ni kweli mkuu yani naamka nalala kama gogo mimiHutomuelewa mleta mada kama huna mtoto yaani mtoto purukushani zake huanza pale akitembea. Ndani ya nyumba huwa inachangamka sana akiwepo mtoto leo kaondoka milele. Nyumba huwa inapwaya sanaa mpaka unaichukia hakika mfiwa pole sana.
Kwioooo
Ni kweli kabisa mkuu niko vipande vipandeManeno mengine ni ya kufarijiana tu ila kuzika mtoto kusikie tu.
Hakuna huzuni kubwa kama kwa baba kumzika mwanae.
Ayubu 1-2Kaka naomba nisaidie mistari ya ayubu katika biblia
Kweli kabisa mkuu! Hii ilinikuta mwezi January, kijana wangu alianza kuhisi maumivu makali sana ya mgongo mpaka kukaa alikuwa hawezi. Akilala nako kuja kuamka ni shida! Yaani ikawa kukaa kwake mpaka aweke mto nyuma ya mgongo.acha kufa akiugua tuu moja haikai wala mbili..
Mzee kanisa la Yesu linakuita nenda kanisani kama uko dar eagt city center kwa pastor katunzi ni sehem sahihi sana kusali....Habari ndugu zangu,
Asante kwa wote mliolia nami katika kifo cha binti yangu mpendwa aliefariki kwa uzembe wa watu wa afya, faraja yenu ilikuwa tiba sana sijaamini JamiiForums kuna watu wana roho nzuri hivi na wanaumia kwa matatizo ya watu.
Maisha baada ya maziko yamekuwa magumu sana muda wote nalia nimeshindwa kurejea kawaida, kwa sasa natamani kufa tu maana naona giza kuna njia yoyote ya kusaidia kuondoka hali niliyonayo?
Naishi peke yangu mama yake tulikuwa hatukai pamoja ila yeye baada ya msiba amehama mkoa kabisa.