Mahusiano yananipa changamoto

unajua wachaga nawapenda kwa sababu ya chachu ya maendeleo, currently am employed but am not satisfied bado ni nadream za biashara haswa kwenye nyanja ya madini,
umeanza vizuri ukaaribu hapa ukitaka kupata mke wacha aje kama muujiza.

Ndoa nyingi zilizodumu waliwapata wenza wao kwa njia ambayo hawakutegemea.

Nb. Mke utakae muoa atakuwa na sifa kuu tatu
1. Utampata mazingira ambayo utarajii kukutana nae
2. Hutompenda mwanzoni
3. Hastahili kujua wewe ni nan at first.

mwisho mkumbushe mungu mke unaemtaka.
 
Mkuu hata mimi yananipa changamoto tutafutane tusaidiane kutatua hizo changamoto
 
yaani umeongea ukweli hapo
 

duuuuh pole sana aisee ..yaan muda ulikokuwa kwenye uhusiano na kupata maumivu haujapishana na wa kwangu..dada kichaga niko hapa ..teeh teeh wasikutishe hao workmate .
 
Muombe Mungu,japo yataka moyo. Ila mie nilisha hachana nayo ata kuyafikiria ! Chakushukuru naona siku zinaenda bila tatizo. Ndo uwa nasemaga Ahsante Mungu.
 

Umeongea kitu ya maana sana mkuu..kama atafuata ushauri wako..hatoumiza kichwa atatulia na kumuomba Mungu na kuyaruhusu maisha mengine yaendelee..ukioa kwa sababu agemates wako wote wameoa utateseka miaka mianane mkuu
 
Ila kwa upande mwingine nilicho jifunza ,kosa la mtu 1 lisikuvunje moyo! Mana utawahukumu wengine kwa makosa yasiyo wahusi si wote wabovu! Utampata mwema na utashangaa mie mwanzo nilikuwa nafikiri labda ni umri lakini lah si kweli ,waweza kuta mtu umri mkubwa lakini hajitambui kimahusiano,yupo yupo tu madamu yupo waweza sema labda kaubwa kwa lengo la kuwaumiza wenzie.
 
Ushauri wangu kwako ni kuwa usiingie katika mahusiano hasa ya ndoa pasipo kumshirikisha Mungu. Omba hekima na uongozi wa Mungu akupatie MTU sahihi.... Sehemu ya ubavu wako.... Usiongozwe na tamaa na yale tuyaonayo kwa MACHO. Mwombe Mungu akuongoze upite katika hatua sahihi vya kuifikia hatma yako ya NDOA.

All the very best....!!!
 

Mithali 31:10-31
10 Mke mwema, ni nani awezaye kumwona?Maana kima chake chapita kima cha marijani.
11 Moyo wa mumewe humwamini,Wala hatakosa kupata mapato.
12 Humtendea mema wala si mabaya,Siku zote za maisha yake.
13 Hutafuta sufu na kitani;Hufanya kazi yake ya mikono kwa moyo.
14 Afanana na merikebu za biashara;Huleta chakula chake kutoka mbali.
15 Tena huamka, kabla haujaisha usiku;Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula;Na wajakazi wake sehemu zao.
16 Huangalia shamba, akalinunua;Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu.
17 Hujifunga nguvu viunoni kama mshipi;Hutia mikono yake nguvu.
18 Huona kama bidhaa yake ina faida;Taa yake haizimiki usiku.
19 Hutia mikono yake katika kusokota;Na mikono yake huishika pia.
20 Huwakunjulia maskini mikono yake;Naam, huwanyoshea wahitaji mikono yake.
21 Hawahofii theluji watu wa nyumbani mwake;Maana wote wa nyumbani mwake huvikwa nguo nyekundu.
22 Hujifanyia mazulia ya urembo;Mavazi yake ni kitani safi na urujuani.
23 Mume wake hujulikana malangoni;Aketipo pamoja na wazee wa nchi.
24 Hufanya nguo za kitani na kuziuza;Huwapa wafanya biashara mishipi.
25 Nguvu na hadhi ndiyo mavazi yake;Anaucheka wakati ujao.
26 Hufumbua kinywa chake kwa hekima,Na sheria ya wema i katika ulimi wake.
27 Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake;Wala hali chakula cha uvivu.
28 Wanawe huondoka na kumwita heri;Mumewe naye humsifu, na kusema,
29 Binti za watu wengi wamefanya mema,Lakini wewe umewapita wote.
30 Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili;Bali mwanamke amchaye BWANA, ndiye atakayesifiwa.
31 Mpe mapato ya mikono yake,Na matendo yake yamsifu malangoni.
 
Thanx
 
Dawa ni kusali na kumwomba mungu akupe Wa kufanana na wewe
 
Tenga muda special kabisa wa kutembelea moshi kutafta mchumba, ukisubiri wachaga wa dar utakesha maana walioko huku wameletwa na waume zao kuolewa.
 
[emoji121]
MKUU,

HILI TANGAZO LIMESHALIPIWA HADI VAT?

TUANZIE HAPO.
 
Point ya mwaka
 
Jisajili CHAPUTA..member wa kudumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…