mahusiano wadau

Parasite

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
613
Reaction score
580
polen kwa majukumu ya hapa na pale.kuna jamaa ametokea kumpenda demu kupita maelezo na demu ameshazimika kimapenzi kwa mshikaji,but kabla ya hapo mshkaji alikua ana demu mwengine ambapo yeye hampendi bali demu ndio analazimisha mapenzi na ndio maana jamaa aliamua kutafuta mwengine yaani yule ampendae yeye.sasa yule demu wa kwanza amemganda jamaa hataki kumuacha kila jamaa anavyojitahidi demu wapi anahofia kumchana laivu kwasababu anaweza afanye kitu kibaya.je wadau mngemshauri nini kijana mwenzetu maoni yenu ni ya muhimu sana??????????????????????????
 
Kwanza samahani wape heshima dada zako kwa kutokutumia neno demu.

Hapo ni yeye mwenyewe kukaa na kuongea na huyo mpenzi wake wa zamani ili waridhie kuachana kwa amani. Sababu hatujui katika mahusiano yao walishafikia katika hatua gani na ni ahadi zipi walishapeana. Pili akae ajitafakari kwa kina kabla hajaanzisha hayo mahusiano ya pili na inavyoonekana bado hajajijua(hajajitambua). Kwani asipoangalia vizuri atakuja kujikuta njia panda. Mapenzi ya mwanzo ni matamu ila mkishakaa na kujuana ndiyo ataona tofauti yake.
 
Hadi shule zifunguliwe week ijayo kizazi cha Big Result Now (BRN) tutapata shida sana
 
Mwambie huyo jamaa aache umalaya

Leo ndo anajifanya hampendi 'demu' wa kwanza?
 
mwambie aoe wote kama dini yake inamruhusu kama haimruhusu basi mmoja akuachie wewe
 
Aafu sio kila aliyepohumu ni kijana mwenzio.! Kuna wengine ni mama na baba zako!
 
"Demu" mchana" haya maneno yamekupotezea sifa ya kupewa ushauri hapa Jf!!
 
yeye aendelee kuwagegeda wote wawili...wala asijipe presha ya kusema amuache huyo demu wa kwanza....wanawake ni burudani ukiwa nao zaidi ya mmoja ndio inapokuwa bonge la burudani!!
 


kama jamaa mwenyewe tu hana maamuzi ushauri utasaidia nini?
 
Kuwa mkweli mbona ni wewe mwenyewe. Cha msingi mueleze huyo mpenzi wako wa sasa ukweli wote na mshauriane cha kufanya. Kama umempenda kweli kama unavyosema tangaza nia. Acha bifu na mpenzi wako wa zamani haina faida kwako.
 
thank you wadau kwa kiasi fulani hoja nyingi zina uzito japo ndugu zangu wengine wako kiutani zaidi tutafika tu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…