Mahusiano sio rahisi hivyo

mamamzungu

JF-Expert Member
Nov 17, 2019
2,374
3,887
Kusema ule ukweli kuachana na mtu ni kazi sana maana itakuchukua muda kumpata mwingine ambae atakupa Furaha na amani

Mwaka 2021 niliachwa muacho safi kabisa yule jamaa aliniandikia sms moja tu

“ Ukikua utajua namna ya kuzungumza na mwanaume sasa hivi utoto unakusumbua”

Ni katika mahusiano niliyoyaamini sana maana kijana alikuwa mkubwa kwangu then alikuwa ananinichukulia kama mdogo wake…. Nilimbembeleza wiki nzima anisamehe ila hakukubali… nikajiapiza tarehe 2/2/2021 ndio mwisho wa kumbembeleza kuomba asiniache kweli jamaa akakataa kunisamehe na Mimi tangu hapo nikafuta kila kitu chake sikumtafuta mpk Leo hii

Nashukuru huwa sibaki single nakaa muda mfupi sana naingia mahusiano mapya… basi ndio katika huku na huku nikakutana na mpzn wangu wa sasa imenichukua mwaka na miezi mpk kumpenda na kuwa huru kwake

Niseme ni moja ya mahusiano ambayo nimekuwa huru Sanaa… sina uoga wa kuzungumza pale anaponikwaza nasema kile nachojisikia kusema… amekuwa kama rafiki kwangu simfichi chochote kunihusu

Niwaambie tu kuliko kuachana ni bora kutengeneza mkaanza upya ni ngumu kumpata mtu wa kuanzA mahusiano mpk mkazoeana

Nipo na stresss jamani
 
Back
Top Bottom