Mimi nadhani ni mambo ya 'digitali'. Kuna mshkaji wangu alipendana na binti, bahati nzuri ama mbaya,upande wa binti mambo safi,kuanzia familia hadi binti mwenyewe,ilhali mshkaji wangu mimi hali yake ni 'tia maji tia maji',familia kama dizaini haikufarahishwa na muunganiko wa wawili hawa ika-set mahari 'karibu na ceiling'. Kwakua wanapendana, 'njiwa' hawa wawili wakatengeneza mpango baina yao,bi harusi mtarajiwa akatoa mzigo kama 95% akamkabidhi mshkaji akatop up 5% akaukabidhi mzigo kwa wazazi wa binti. Hali kadhalika kama ilivyotarajiwa send-off ilikua funika bovu,harusi 'mchele mchele', bi harusi akawashirikisha 'ndugu waaminifu' wakatema kitu kama 6M harusi 'mchele-mchele' ukapungua picha likawa clear wakaoana! So, kusaidiana kupo kama nia ni njema na mapenzi ni ya dhati. By the way, si 'wanawake nao wanaweza ama'?