Desidii
JF-Expert Member
- Oct 2, 2007
- 1,201
- 86
Kwanza habari zenu nimewamisi sana kitambo sijatia timu hapa.
Hii imenitokea mimi mwenyewe na kunikosesha raha kabisa.
Wiki kama mbili hivi tulipata barua ya uchumba ya mtoto wa dada yangu tunaishi nae kwa wazazi wangu baada ya dada kufariki. Wazazi waakaijibu vizuri haikuchukua muda tukaambiwa mahari inaletwa wiki inayofata, tukawakubalia nilihusishwa nikiwa kama mwanafamilia na mtoto wa mwisho kuzaliwa na ambaye naishi na kuwatunza wazazi. Nilikuwa na mawasiliano na mtoto wangu kwa karibu na huwa ni rafiki ndugu haya tukaandaa kila kitu nikashangaa usiku wa kuamkia hiyo Jumapili ambayo ndo wanaleta mahari ananimbia Mama Mdogo niazime tsh.... Nikamuuliza za nini? Jibu nililopata nusu nizimie eti mkwe kapungukiwa mahari mie kijasho kikanitoka na kumuulizaa kulikuwa na haja gani ya kukimbilia kuja wakati hamjajipanga? Hakuna jibu la kueleweka hata chembe nikanyamaza maandalizi yanaendelea akaona haitoshi kampa namba ya simu yangu huyo mkwe aniombe nikashangaa sana tena sana nikaona huruma nikamwazima huku nikiwa sielewi ni nini maana ya hii. Mimi kama kawaida ya kutaka kujua kwanini iwe hivi nikachukua simu yake nakuiangalia na kukuta mpango umepangwa kunidanganya mimi. Wakati nimeshatoa tayari iliniudhi sana na kumuuliza mwanangu why unanifanya mimi mjinga? Majibu anayonipa namuonea sababu mama yake amekufa najiuliza jukumu la kutoa mahari ni la nani jamani? Ama mimi ndo mshamba sana au bado nina mambo ya kale?? Nisaidieni plz