Mahakama yazuilia mali ya Neymar

Mkoroshokigoli

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
14,594
5,579
Mahakama moja ya Brazil imepiga tanji mali ya mchezaji nyota wa Barcelona, Neymar.

Mahakama hiyo iliopo Sao Paulo ilitangaza kuwa inatoa waranti ya kuzuia mali yenye thamani ya takriban dola milioni 50 ya mchezaji huyo wa Brazil.

Mali hiyo inashirikisha ndege,jahazi la kifahari na Mali nyengine.

Neymar mwenye umri wa miaka 23 ametuhumiwa kwa kukwepa kulipa kodi kati ya mwaka 2011 na 2013 na anakabiliwa namshataka ya kujibu.
Amekana kufanya makosa yoyote.

Miongoni mwa mali zilizozuiwa ni kampuni tatu zinazomilikiwa na familia yake.

Waendesha mashtaka wanamtuhumu Neymar kwa kuanzisha kampuni ambazo zilimsaidia kulipa kiwango kidogo cha ushuru.

Wanataka alipe dola milioni 16 kama kodi ambayo haikutangazwa.
Mahakam hiyo iliagiza mali yake kupigwa tanji ili kuhakikisha kuwa anafanya malipo hayo pamoja na faini.

Hatahivyo Neymar anaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo wa mahakama na kwamba sio rahisi kwa yeye kuhudumia kifungo,kulingana na mkaguzi mmoja wa maswala ya fedha.sosi
Bbc
 
Mascherano, Lonely Mess na Neymar(Barka) ni wakwepa kodi wakubwa na dunia inajua

Ingekuwa Bongo Magu angeshatumbua majibu fasta...
 
Ingekuwa Bongo Magu angeshatumbua majibu fasta...
Mpaka sasa ametumbua WAKWEPA KODI wangapi wenye hadhi ya Neymar? Zaidi ya kupambana na watendaji tu, na hao wakwepa kodi kuwapigia magoti na kuwapa muda walipe kisiri siri.

Nchi za wenzetu hawana UTANI na kitu kinaitwa KODI haijalishi una hadhi gani utalipa na unaweza kwenda jela. Jaribu pia kutoa au kuchukua RUSHWA halafu ubainike!
 
Hapa angepewa siku 7
 
Mascherano, Lonely Mess na Neymar(Barka) ni wakwepa kodi wakubwa na dunia inajua

Ingekuwa Bongo Magu angeshatumbua majibu fasta...
Wenzetu nchi wanaendesha kwa sheria sio kukurupuka. Hii kazi ya mahkama Raisi haingilii vitu kama hivi
 
Duh! anamiliki mali yenye thamani ya dola million 50 halafu kodi anayotakiwa kulipa ni dola million 16
 
Back
Top Bottom