Mahakama Yawataka Wabunge Halima Mdee na Mwita Waitara kuheshimu taratibu za kisheria


TataMadiba

TataMadiba

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2014
Messages
9,659
Likes
3,998
Points
280
Age
35
TataMadiba

TataMadiba

JF-Expert Member
Joined Feb 7, 2014
9,659 3,998 280
1-1-jpg.363059

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imetoa onyo kwa Wabunge Halima Mdee (Kawe) na Mwita Waitara (Ukonga) kwa kushindwa kufika mahakamani kusikiliza kesi inayowakabili dhidi ya kumjeruhi Katibu Tawala wa jiji, Theresia Mbando.

Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi na leo kesi hiyo ilipangwa kusikilizwa maelezo ya awali dhidi ya washtakiwa.

Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Esterlia Wilson alidai kuwa kesi hiyo ilipangwa kusikilizwa maelezo ya awali lakini washtakiwa Mdee na Waitara hawapo mahakamani.

Utetezi ulidai kuwa Mdee ameshindwa kufika mahakamani kwa kuwa amesafiri kwenda nchini Canada na Waitara ni mgonjwa.

Hakimu alisema sababu zilizotolewa na upande wa utetezi hazina mashiko kisheria kwa kuwa wameshindwa kuwasilisha vielelezo vya kuithibitishia mahakama kwanini washtakiwa wameshindwa kufika kusikiliza kesi yao.

“Kama kweli mshtakiwa Waitara ni mgonjwa upande wa utetezi mlipaswa kuwasikilisha vyeti mahakamani na kuhusu mshtakiwa Mdee aliyesafiri kwa safari zake binafsi kwenda Canada, siyo sahihi tunapaswa tuheshimu hizi taratibu ili kila kitu kifanyike kwa haki ya pande zote” alisema Hakimu Shahidi.

Mbali na Mdee na Waitara, wengine ni, Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea , Diwani wa Kata ya Tabata Kimanga, Manase Njema , Diwani wa Kata ya Kimara, Ephrein Kinyafu na mfanyabiashara Rafii Juma.

Wengine waliounganishwa katika kesi hiyo ni, Diwani wa Kata ya Segerea Edwin Mwakatobe (31) na Mkazi wa Tabata Edwin Mwaipaja (40).

Katika kesi ya msingi, ilidaiwa kuwa Februari 27, mwaka huu katika Ukumbi wa Karimjee, Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam walimjeruhi Theresa Mbando na kumsababishia maumivu mwilini mwake.

Washtakiwa hao walikana mashtaka hayo kwa nyakati tofauti na upande wa Jamhuri ulidai upelelezi wa kesi hiyo umekamilika, uliomba tarehe nyingine ya kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali.

Hakimu alisema kesi hiyo itasikilizwa maelezo ya awali Julai 27, mwaka huu, dhamana ya washtakiwa inaendelea.
 
N

nkongu ndasu

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2013
Messages
22,518
Likes
3,766
Points
280
N

nkongu ndasu

JF-Expert Member
Joined Jan 19, 2013
22,518 3,766 280
duh.....
 
babumapunda

babumapunda

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Messages
4,100
Likes
2,103
Points
280
babumapunda

babumapunda

JF-Expert Member
Joined Dec 21, 2012
4,100 2,103 280
hii nchi ya ajabu sana,aliefoji hati ya mashtaka hivi mpaka leo hajapelekwa mahakamani???kama ni hivyo basi serekali hii ni hopeless
 
Freeland

Freeland

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2012
Messages
14,473
Likes
6,771
Points
280
Freeland

Freeland

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2012
14,473 6,771 280
aiseee
 

Forum statistics

Threads 1,235,280
Members 474,471
Posts 29,216,594