Mahakama yatupilia mbali kesi ya Mwakalebela kupinga Ubunge wa Peter Msigwa

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
1.jpg


Mahakama Kuu Kanda ya Iringa imetupilia mbali kesi ya kupinga matokeo yaliyompa Ubunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema), iliyofunguliwa na aliyekuwa mpinzani wake kwenye Uchaguzi huo, Frederick Mwakalebela (CCM).

Mahakama hiyo pia imeamuru Mwakalebela kumlipa Mchungaji Msigwa gharama za kesi hiyo iliyofunguliwa mwaka jana na kupata usajili wa mahakama hiyo Novemba 30.

Katika shauri la msingi la kesi hiyo namba 5 ya mwaka 2015 ya kupinga matoke, Mwakalebela aliwatuhumu Mchungaji Peter Msigwa na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Iringa Mjini, Ahmed Sawa kwa kukiuka sheria na taratibu za uchaguzi hali iliyopelekea yeye kupata matokeo mabaya yasiyo halali.
 
Sasa kama alijua alipata matokeo mabaya alienda mahakamani kufanya nini wenzake wenje na kafulila wameenda mahakamani na form zinazoonyesha wao ndio washindi ye anaenda mahakamani huku akijua ameshindwa
 
Back
Top Bottom