Shirika la ndege la Etihad leo limekaribisha hukumu ya mahakama ya juu ya utawala mjini Luneburg, Ujerumani ambapo mahakama imepinga hukumu ya awali na hivyo kuiruhusu Etihad kuendeleza safari zake 26 kati ya 31 za ‘makubaliano’ kati yake na Airberlin katika kipindi cha baridi kinachoisha Machi 26, 2016.
Mahakama ilikubali kwamba ‘makubaliano’ 26 kati ya 31 yaliyopendekezwa ni halali kisheria ukijumuisha na mengine 50 yaliyopitishwa na Airberlin, mapendekezo 76 kati ya 81 yamepitishwa moja kwa moja, ikiwa ni asilimia 94 ya mapendekezo yaliyowasilishwa awali.
Maamuzi haya ya mahakama, juu ya makubaliano ya huduma za anga kati ya Umoja wa nchi za Falme za Kiarabu na Ujerumani yanamaanisha kwamba shirika la Etihad litaendelea na safari zake hata baada ya ratiba yake ya msimu wa baridi
Rais na Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Etihad, James Hogan, alisema: “Tumeridhishwa na hukumu iliyotolewa na mahakama kuhalalisha asilimia 94 ya makubaliano.“Hukumu hii ni ushindi kwa wateja na wapinzani wetu waliopo Ujerumani.
“Tunaendelea kuungana na mshirika wetu, Airberlin, na tutaongeza juhudi zetu mara mbili ya awali ili kuleta ushindani mbadala na mkubwa kwa shirika la ndege la Lufthansa, ambao kwa sasa ndio wametawala sana anga za Ujerumani.’
“Tungependa kuwatia moyo wateja wetu waliopo Ujerumani waendelee kuwaunga mkono Airberlin na wafanyakazi wake 8,000 ambao kwa njia moja au nyingine wameathirika na shambulio endelevu juu ya biashara yao”