Kachanchabuseta
JF-Expert Member
- Mar 8, 2010
- 7,269
- 675
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mjini Dar es Salaam, imemwachia huru Naeem Gire aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya kughushi na kuwadanganya serikali kuwa mitambo ya Richmond ina uwezo wa kufua megawati 100 za umeme.
Gire ametoka kizimbani akichekelea baada ya hakimu wa mahakama hiyo, Waliarwande Lema , kutamka kuwa anamuona hana kesi ya kujibu kutokana na ushahidi uliofikishwa mahakamani na serikali kushindwa kumridhisha ili amuone kuwa na kesi ya kujibu.
"....Baada ya kupitia ushahidi katika vipengele vyote nimeona kuwa hakuna ushahidi wa kutosha uliowasilishwa kuridhisha kumuona mshitakiwa ana kesi ya kujibu...kesi hii ni miongoni mwa kesi kadhaa ambazo huletwa mahakamani na kisha kuitwisha lawama mahakama", alisema Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Waliarwande Lema."
Nasubiri Mama Foxy, MS na GeniusBrain waje wacomment kwanza!![/QUOTE
wapo kwenye sherehe ya FF kutumiza miaka 30 ya ndoa
Serikali yetu kama inataka mhalifu wao alindwe wana mbinu nyingi sana, kwani system yetu ya sheria ni kwamba serikali ndiyo mshitaki mkuu kwa kesi zote za jinai.
Hivyo basi kwa kutimiza uminywaji huo wa haki wanapeleka mahakamani mshitakiwa siyo, au mashitaka siyo, au mashahidi siyo, au ushahidi siyo!
Mara nyingine hata mahakimu wawe waadilifu namna gani -- wanachezewa tu na serikali katika kamchezo ka namna hiyo! Serikali inayo uwezo wa hata kuiondoa kesi iwapo itaona mhalifu wao anaelekea kwenda na maji.
maigizo yanaendelea