Mahakama yamwachia huru Naeem Gire wa Richmond

Kesi yenye maslahi makubwa kwa nchi kutupwa on a submission of no case to answer ni dhihaka kwa watanzania.

Mkuu wa mashitaka na au takukuru hawakufanya homework yao sawsawa, wameiangusha nchi kwa hilo.

Njia pekee ni wao kujiuzulu kwa kushindwa kazi
 
Mahakama yamwachia Gire wa Richmond
Send to a friend
Thursday, 28 July 2011 21:32


Nora Damian
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru mfanyabiashara Naeem Gire aliyekuwa anakabiliwa na kesi ya kughushi na kutoa taarifa za uongo kuhusu kampuni ya Richmond. Uamuzi huo ulitolewa jana na Hakimu Mkazi Wariyalwande Lema aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo. Hakimu Lema alisema upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha kesi dhidi ya mashtaka waliyomshtaki nayo Gire.
Alisema ushahidi wa upande wa mashtaka ulikuwa ni dhahifu na kwamba usingeweza kumfanya mshtakiwa huyo ajitetee. “Naiondoa kesi hii chini ya kifungu namba 230 cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai kwasababu upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha mashtaka dhidi ya mshtakiwa,”alisema Hakimu Lema.

Hakimu Lema alisema hakuna sehemu yoyote ambayo mshtakiwa huyo aligushi na kwamba vitu vyote vilifanywa na Mohamed Gire ambaye ni kaka wa mfanyabiashara huyo.

Baada ya uamuzi huo, upande wa mashtaka kupitia kwa Wakili wa Serikali, Shadrack Kimaro ulisema utakata rufaa kupinga hukumu hiyo. “Tunaomba tupewe nakala ya mwenendo wa kesi na nakala ya hukumu kwa ajili ya kwenda ngazi za juu zaidi,”alisema Kimaro.
Gire alikuwa akidaiwa kuwa, Juni, 2006 jijini Dar es Salaam alitoa taarifa za uongo kwa wajumbe wa timu ya majadiliano ya Serikali, kuwa Kampuni ya Richmond LLC ya Texas, Marekani, ina uwezo wa kuzalisha umeme ili apewe zabuni.

Mfanyabiashara huyo pia alikuwa akidaiwa kuwasilisha hati ya nguvu ya kisheria iliyotolewa Machi 3, 2006 ikimuonesha kuwa aliruhusiwa na Mwenyekiti wa kampuni hiyo, Hemed Gire ambaye ni kaka yake kufanya kazi za kampuni hiyo hapa nchini. Mwisho.
 
maswali ambayo DPP hawezi kuyajibu ni pamoja inakuwaje wale waliopo serikalini walioiteua timu ya washauri na ile timu ambayo inakiuka sheria ya manunuzi mbona wapo mtaani warandaranda tu.........................................hivi unaposhauriwa ujambazi ukauafiki na kuutekeleza yawaje wewe DPP akuone u msafi..................................................kesi hii kamwe haitafanikiwa serikali kwa sababu lengo la DPP ni kumfurahisha yule aliyemteua ambaye ndiye mmiliki halali wa Richmond....................
 
Kwa maneno mengine hakimu anaiambia serikali kamata Mohamed Gire na sio Naeem Gire bado hilo li wakili la serikali linanang'ang'ania kuendelea na Naeem Gire. Basi kwa maana hiyo kama hakuna kesi basi Lowassa yuko safi!!

Je, huyo hakimu hajapewa kitu kweli?

Hivi kweli nchi hii ina mihimili mitatu kweli ambayo iko sawa na si rahisi kuingiliana? Nilisoma sehemu kuwa mahakama ni mkono state na pia Rais anaweza kulivunja Bunge, sasa je hayo ya usawa sio maigizo kweli?
 
Sasa Mr Gire aende mahakamani akadai fidia. Things must get even worse before getting better. Waendelee tu kutukera na michezo yao ya kuigiza.

Kama unasema kweli vile mkuu. Sitaona ajabu ikitukia.
Hapo ndipo ninapoikubali hotuba ya Godbless Lema ya jana huko mjengoni.
Serikali legelege bwana ... hata mashtaka yanakuwa kama ya watoto wakichongeana kwa wazazi wao. Kwanza wanakubaliana: "Usije kusema eeh". Halafu wazazi wakija mmoja aliyeonywa anaanza kusema; "unadhani nimesema?". Aaa! Halafu siri inatoka.
Siri zao zitatoka tu ... Ngoja wananchi (ambao ni wazaz)i wakae sawa kudai haki zao
 
Ina maana Richmond Imeshinda kesi. sasa watuhumiwa wengine upande wa serikari hawakuwajibika kihalali?
 
naona siku hizi itabidi tuwe tunaleta waendesha mashtaka toka nje, yaani tubinafsishe idara ya mwendesha mashta, maana inaonekana hawajui au hawako huru, halafu lushuwi atakuja na zake kwamba vyama mbadala wachochezi
 
Nahisi kuna dalili za taasisi fulani kutuma michnago ktk hiyo kesi ili tuwakilishwe vizuri!
 
Ina maana Richmond Imeshinda kesi. sasa watuhumiwa wengine upande wa serikari hawakuwajibika kihalali?

Tatizo lilikuwa ni uwaziri mkuu........tatizo ni uwaziri mkuu. Haya ya kumpeleka mahakamani Naeem Gire ni ``cover`` tu ya project nzima.
 
Tatizo lilikuwa ni uwaziri mkuu........tatizo ni uwaziri mkuu. Haya ya kumpeleka mahakamani Naeem Gire ni ``cover`` tu ya project nzima.

What comes around goes around! As long as Richmond ni mradi wa JK, hakuna kesi yoyote dhidi ya Richmond itakayoweza kushinda mahakamani!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom