Bukanga
JF-Expert Member
- Dec 13, 2010
- 2,857
- 1,936
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma chini ya Hakimu Mfawidhi Silvester Kainda ametupilia mbali kesi dhidi ya David Kafulila iliyofunguliwa tangu mwaka 2014 kwa kosa mwaka 2013 kwamba alimdhalilisha D.C. wa uvinza wakati huo Bi Hadija Nyembo.
Kwamba uamuzi wake wa kuagiza polisi kuchoma nyumba za wakulima disemba2012 kitongoji cha ruhama kijiji cha bweru kata ya Itebula wilaya ya uvinza kwa madai ni hifadhi ilitokana na weledi wake mdogo wa sheria na kwamba ndio madhara ya JK kuteua maDC wenye viwango sawa na mashangingi wa mtaani.
Kwamba Kafulila alijenga hoja hiyo kwa mantiki kwamba kitongoji husika hakikuwa hifadhi kwani kimo kwenye orodha ya vitongoji kwa mujibu wa tangazo la serikali GN no205 la 2009.
Katika uamuzi wake Hakimu Silivester Kainda alisisitiza kuwa kutokana na upande DPP kushindwa kuleta mashahidi kwa zaidi ya siku60 sasa, Mahakama imeamua kufuta kesi hiyo na kumwachia huru mshitakiwa David Kafulila kuanzia leo January 19, 2016.
Kwa uamuzi huu, David Kafulila atabaki akikabiliwa na kesi ya kuhamasisha wananchi wasichangie ujenzi wa maabara mwaka 2014, kesi ambayo Leo imendelea na kuahirishwa mpaka January 25. Katika kesi hiyo mashahidi wawili wamekamilisha ushahidi wao Leo kwa Hakimu huyo huyo katika mahakama hiyohiyo ya Hakimu Mfawidhi Kigoma.
Mbali ya kesi hizo katika Mahakama hiyo ya Hakimu Mkazi Kigoma, David Kafulila amebaki akikabiliwa na kesi katika Mahakama ya Kisutu Dar ambapo Kampuni ya IPTL, PAP na Mkurugenzi wake Harbinder Sigh Sethi wamemfungulia kesi Kafulila wakimdai shilingi milioni100 kwa madai ya kwamba alichafua jina la Mkurugenzi hiyo na kampuni hizo katika sakata la ESCROW. Kesi hiyo inaendelea katika Mahakama ya Kisutu Chini ya Hakimu Mcharu na ilifunguliwa baada ya kutupwa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar ambapo Kafulila alidaiwa 310bilion kutokana na hoja kwamba alitumia lugha za kumchafua Sethi na Makampuni yake