Zahir Salim, Fisadi Mtoto na wengine wote wanaomsujudia 'Rais' Rostam:
Hivi mnaamini kweli Marando -- mwanasheria wa Kubenea kashindwa na Rostam?
Haiwezekani! Kuna kitu hapa kinachezwa: Kwa wale waliobahatika kuiona hiyo hukumu ya jaji Makaramba wataona ni dhahiri Rostam kachezewa mchezo, maana anadhani yeye (RA) ni mjanja kuliko Watanzania wote. Sherehe anazofanya kupitia magazeti yake na Habari Leo ni temporary tu. Ngoma bado mbichiiiiii!
Kategewa ndoano na imemnasa barabara mdomoni -- kwa hiyo bado analo la Richmond, lazima aanikwe kwa njia za haki.
Hukumu yenyewe ya kurasa 3, ambayo 'hukumu' hasa ni mistari 13 tu haiwezi ikawa ndiyo hukumu ya shauri hilo, kwani shauri halikusikilizwa kabisa. Akina Mrando hawakuwa wanafika shaurini kwa makusudi, kwa sababu maalum: waligutuka kwamba hawawezi kupata haki chini ya jaji huyo -- tena jaji mmoja.
Kwa hivyo rufaa nadhani itakuwa imewasilishwa -- ya kutaka shauri lisikilizwe na jopo la majaji watatu -- na sheria za kesi za madai inaruhusu hivyo. Na hapo ndipo RA atagundua kuwa kama yeye anajua huu, wengine wanajue hii. Ndipo atakapofahamu kwamba maharage siyo mboga bali ni dawa ya tumbo tu!
Wana-JF Ngoma bado mbichi nawakakishieni -- RA bado yuko kitanzini tu kuhusu Richmond, watanzania tuzidi kumbana huyu hadi kieleweke. Hata akisajili mawaziri wangapi na kuvinunua vyombo vyote vya habari vya serikali, umma ni lazima uibuke mshindi dhidi ya mdosi huyu aliyetuibia mamilioni!