Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 15,999
Jaji wa mahakama kuu kitengo cha ardhi,Mh.Fredrick Sanga leo tar.22.4.2016 ameamuru kubomolewa kwa nyumba maeneo ya segerea bila fidia.Ikumbukwe wananchi 2619 walingua kesi kwa niaba ya wakazi zaidi ya 4000.
Pigo hili kwa wakazi wa mabondeni.
======================
Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi imetupilia mbali kesi ya walalamikaji waliojenga maeneo hatarishi kwa maisha ya binadamu katika jimbo la Segerea jijini Dar es Salaam kwa kukosa baadhi ya majina ya walioomba kuwakilishwa katika kesi hiyo.
Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi imetupilia kesi ya wakazi 2619 ya kupinga kubomolewa nyumba zao bila kulipwa fidia yoyote na serikali kwa wakazi zaidi ya elfu nne wa eneo hilo mara baada ya wakazi hao kukosa majina na sahihi za wananchi walioomba kuwakilishwa katika kesi hiyo.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Jaji Fredrica Mgaya wakati shauri hilo amesema kesi hiyo imefutwa kwa kukosa majina na sahihi za watu wanaotaka kuwakilishwa na watu wanane walioshauliana kuwa watawasimamia katika kesi hiyo ya bomoabomoa ya wakazi wa jimbo la Segerea.
Akisoma maamuzi ya wakili wa serikali Gabriel Malata amesema kuwa walalamikaji hawana kibali au viapo halali vya wakazi hao kuomba kuwakilishwa na watu walioteuliwa kuwasimamia katika kesi yao ya kubomolewa makazi yao.
Pia Jaji Fredrica Mgaya ameiomba serikali kutoa elimu kwa wakazi wa maeneo ya mabondeni ili wajue athari zitakazowakuta kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Chanzo: Michuzi