Mahakama ya mafisadi au Division ya Mafisadi.

Mahakama ya mafisadi au Division ya Mafisadi.

moyAfricatzz

Member
Joined
Mar 7, 2016
Posts
56
Reaction score
29
Habari za jion wana jamvi,
Nakumbuka vizuri Mhe,Rais alitoa ahadi ya uanzishwaji wa mahakama ya mafisadi ili kufanikisha uharakishwaji wa kusikilizwa kesi za mafisadi na mhe,Hussein Bashe mbunge wa Nzega aliwahi kumwambia kwamba atakuja kumkumbusha mhe Rais kuhusu uanzishwaji wa mahakama hiyo,hata msemaji wa ccm ole sendeka juzi alisema wapinzani wanaogopa na akataja moja ya sababu ni ahadi ya uanzishwaji wa mahakama hii ya mafisadi..
Mwezi kama mmoja uliopita katika taarifa habari ya kituo cha ITV mahakama ilikua inazindua jengo jipya litakalokua linatumika na hiyo mahakama ya mafisadi..kilichonichanganya mimi binafsi ni kitendo cha chief justice mhe jaji othman chande kusema litakua jengo la division'(divisheni)ya mafisadi katika mahakama kuu..
Sasa basi,divisheni(division)za mahakama kuu zinazojulikana mpaka sasa ni tatu,divisheni ya kazi(labour division),divisheni ya ardhi(land division) na divisheni ya biashara (commercial division)..na hizi zote ziko chini ya mahakama kuu ya Tanzania(High Court)
Sasa tunajua katika uanzishwaji wa mahakama hapa Tanzania lazima kuwe na utungwaji wa sheria ili kusapoti uwepo wa mahakama hiyo,ndo mana mahakama ya mwanzo na wilaya zipo kwenye Magistrate Court Act section 17,18 na 20.Na pia mahakama kuu ya Tanzania inaongelewa kwenye katiba yetu ya Tanzania kwenye article 108(1),High court of Zanzibar pia iko kwenye Article 114 ya katiba ya Tanzania ya mwaka 1977,pia Article 117 ya katiba yetu inasema"There shall be a court of Appeal of the united Republic,(to be referre to in short as 'the court of Appeal)which shall have the jurisdiction of the court of appeal as provided in this constitution or any other law.
Hiyo ni mifano michache inayoonyesha kwa kifupi kwamba uanzishwaji wa mahakama yeyote hapa Tanzania lazima upewe mashiko na sheria husika ..
Mahakama kuu inashughulika na makosa mengi lakini hasa ya jinai(criminal) na ndo mana tuliona hata baadhi ya mawaziri wastaafu wa kipondi cha mkapa walishtakiwa na kupewa adhabu ya kifungo..
Makosa kama utakatishaji pesa(money laundry),economic sabotage(uhujumu uchumi)yanaweza kupelekwa mahakama kuu na kufikiwa maamuzi pale..kifupi hata hawa mafisadi ambao bado hawajashitakiwa ,wangekamatwa na ushahidi ungepelekwa na wangefunguliwa kesi pale mahakama.kuu.
Maswali yangu ni kwamba kama ni uanzishwaji wa "mahakama ya mafisadi" imeanzishwa kwa kifungu kipi cha sheria?je hiyo mahakama inapewa nguvu na sheria ipi??na kama mahakama kuu ina uwezo wa kusikiliza na kuhukumu mafisadi wenye kesi za jinai za kujibu kwa nini wasikamatwe na kupelekwa hapo?ya nini kuanzisha mahakama mpya??
Au nishawishike kuamini si uanzishwaji wa mahakama.ya mafisadi bali ni "uanzishwaji wa divisheni mpya ya mafisadi ndani ya mahakama kuu"???
Which is which???
Msaada please...!!!!!
 
Hakuna atakae jitokeza kuchangia hapa...wako busy na ukuta pamoja na kazitu
 
Hapa kitakachoanzishwa Ni divisheni, kusema divisheni Ni sawa Tu Na kusema mahakama kuu ya mafisadi, hivi karibuni yalifanyika marekebisho mbalimbali ya sheria, katika marekebisho hayo Kuna sheria za uhujumu uchumi ziliongezewa kipengele cha uanzishwaji wa hiyo mahakama (establishment clause) Na jaji mkuu (CJ) akapewa mamlaka ya kuunda hiyo divisheni.
 
Back
Top Bottom