Mahakama ya Katiba vs Ufisadi; ipi ianze?

Baraghash

JF-Expert Member
Dec 18, 2012
2,713
1,789
Nadhani palikuwa na haja ya kuanzishwa Mahakama ya Katiba kwanza kuliko hiyo ya ufisadi
1 kwa vile kila mtu ni fisadi katika mfumo huU wa utawala wa CCM. Mahakama ya ufisadi haiwezi kufanya kazi na itaishia mafisadi kupewa adhabu ya kufanya kazi ya jamii.
2.Mahakama ya Katiba inahitajika sasa kuliko wakati mwengine wowote ule. Umefika wakati wanasiasa walioko madarakani wanavunja Katiba wapendavyo na hakuna hatua zinazo chukuliwa kwa vile hakuna chombo cha kushughulikia uovu , zaidi ya kuwaruhusu wanasiasa kutetea uovu huo.
3. Mahakama ya Katiba inaweza pia kusikiliza kesi za ufisadi na utumiaji mbaya wa madaraka
 
Kwani ilani ya walioko madarakani inasemaje? kwani rais anasemaje?
 
You are very right.

Imagine kama tungekuwa na mahakama ya kikatiba, naamini hata huu mkwamo wa kisiasa unaoikabili Zanzibar kwa sasa ungeweza kuwa resolved.

Kwa kuwa wanasheria mahiri wa mahakama hiyo wangeweza kufanya tafsiri ya sheria kwenye Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 na ile sheria ya uchaguzi ya Zanzibar, ili kubaini kama yale mamlaka aliyodai anayo Jecha kama kweli anayo au huyo Jecha 'alijikurupukia' tu kuufuta uchaguzi huo.
 
Katiba ndio sheria mama bila ya katiba mpya kupatikana hizi mahakama hazitafanyakazi vizuri.KATIBA YA WARIOBA NDIO INAFAA KWA RAIS MAGUFULI ILI AWEZE KUTUMBUA MAJIPU VIZURI BILA YA LAWAMA.
 
Naunga mkono hoja. Mahakama ya katiba imemnyoosha Rais Zuma huko Afrika Kusini.
Na hiyo hiyo imesema ni uvunjifu wa katiba askari Polisi kuingia kwa nguvu Bungeni. Kwa kweli hata sie tulihitaji sana kuwa na mahakama ya katiba mapema sana ili kuweka sawa uhuni unaoendelea.
Hivi kwani hiyo mahakama ya mafisadi sii itakuwa inahukumu kwa sheria ambazo ndio hizi hizi zinazotumika kwenye mahakama ya kawaida? Sasa tunabadili sheria au tunajenga mahakama za mafisadi?
 
Back
Top Bottom