Mahakama inaingiliwa na nani?

Aaronium

Senior Member
Oct 31, 2011
129
9
Ndugu wapendwa let me salute you once again!

Kumekuwapo na malalamiko kutoka kwa wadau mbalimbali ya kwamba mahakama imekuwa ikiingiliwa sana haswa kwa kipindi cha hivi karibuni, kuhusiana na kesi ya ndugu Mh. Lema mbunge wa Arusha mjini!

Swali ambalo linahitaji majibu ni hilo hapo juu, lakini kuna dondoo za kuelekea katika majibu mazuri na ya kuridhisha pia kuleta muafaka.....
1. Mahakama ni mhimiri mmojawapo katika dola hii ambao unahitaji kufanya kazi kwa uhuru kabisa kutofungamana na upande wowote! iwe jamii, watu binafsi mmoja mmoja labda na pia serikali.
2.Uhuru huo unaendelea mbali zaidi na kuihusu yenyewe kama mhimili kutafakari amri, maagizo, maelekezo yanayotolewa na serikali na kuyakataa kama ikibidi iwapo itaona kwamba anaingilia uhuru wake...... well just to mention a few,

Mkuu wa mkoa anaiagiza mahakama kutotekeleza ombi la wana-CDM kuhusu dhamana ingawaje pia mahakama ililizungumza vizuri pamoja na wanazuoni, chama cha majaji wastaafu ati CDM inataka kuiburuza mahakama, what about mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya etc ambao walitoa maelekezo ati kwamba huyu ndugu kwa sababu anakiburi basi abakizwe mpaka siku ya kutajwa kesi?

Pili, mahakama ya rufaa with the famous walk away, pale serikali ilipopinga award aliyopewa Ndg. Mtikila kuhusu haki ya mgombea binafsi, ambapo ni wazi kwamba there was a strong influence from the government ambayo mkuu wake ambaye ni rais, anakaa juu ya sheria na vyombo vyote ambavyo ameteua watendaji wake ambao wameapa kiapo cha utii mbele yake! Na wote mnakubaliana na mimi bila shaka adhabu ya kutomtii Mh. Rais ni kunyongwa mpaka kufa, je hawa ndugu labda iwekwe sawa bila kuficha nyuso, wanao ukweli wowote wanaousimamia kama siyo kujaribu kumfurahisha tu huyu mheshimiwa? Jaji mmoja maarufu ambaye anapendeza na ukweli wake ni Mh.Jaji Augustino Ramadhani, kusema kwake kwamba matokeo ya urais yanaweza kupingwa mahakamani kulimgharimu nafasi yake amini usiamini lakin bravo, YOU HAVE DONE YOUR NATION A GREAT SERVICE AND THANK YOU!..... Wale mliobaki na kulewa madaraka mtaishi uongo na kujutia mioyoni mwenu mpaka mtakapoondoka hapa duniani...you live a lie, kwani kiini cha mahakama hiyo kudharaulika na kuingiliwa ni misimamo ya watendaji wake wakuu ambao hawana sifa za kutosha na wanateuliwa kushika nafasi hizo kwa kiwango kikubwa kwa sababu ya ahadi zao za kutetea hicho chama!
 
Back
Top Bottom