Mahafali ya 48 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

senzighe

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2012
Posts
2,376
Reaction score
1,957
Tangazo hili la mahafali limesainiwa na makamu mkuu wa chuo .Linaonyesha idadi kubwa ya wahitimu watarajiwa wa kike kuliko ile ya wanaume.Je lina ukweli ? Ukilitazama jedwali la wahitimu katika upande wa asilimia linaonyesha mkanganyiko katika jinsia..Je tangazo hili kweli limetoka chuo kikuu kwa wasomi ?
 
Attachments

Awamu hii ya utawala ndio nimetambua na kuielewa nguvu ya PhD.
 
Haha nilikuwa nimekuandalia dongo kuwa kuna dhambi gani wanawake wakiwa wengi....ni kweli wamechemka bwana. Either wamechanganya idadi ya huku wameweka huku au wamekosea kuziweka zile asilimia

Tangazo zima limeingia dosari. Limekua batili
 
Kumbe masters inaitwa shahada ya umahiri nilijua inaitwa Shahada ya Uongozi/unahodha etc
 
Hii document mbona haifunguki?
 
Haha nilikuwa nimekuandalia dongo kuwa kuna dhambi gani wanawake wakiwa wengi....ni kweli wamechemka bwana. Either wamechanganya idadi ya huku wameweka huku au wamekosea kuziweka zile asilimia

Named as the best university in the country
 
Ni kweli. Kwa nini unalitilia mashaka? Unafikiri tangazo kama hilo limepitiwa na watu wangapi au mara ngapi kabla ya kutolewa hadharani? Tatizo ni kuwa fikra zetu mara nyingi zinatushawish tubaki pale pale wakati mambo yanabadilika kila siku.
 
Wenye akili timamu wameshaona tatizo.Acha kubwabwaja.
 
Hata juzi wakati nimehudhuria kongamano la uchumi kwenye kijitabu cha ratiba waliandika kutakuwepo na Mada NNE(4) cha ajabu walipotaja kwenye orodha zikawa tano na wawasilishaji walikuwa watano ndo nikakumbuka shairi la Atieno yooo(in nshomile's idiolect).
 
Sasa ubatili wake uko wapi? Mbona mnamatatizo hivi?

Umesoma hoja inayojadiliwa mkuu?
Kwa mujibu wa hilo jedwali, wanawake ni wengi kuliko wanaume, lakini upande wa asilimia unaonyesha idadi ndogo ya wanawake. Hilo kwako sio tatizo?
 
Umesoma hoja inayojadiliwa mkuu?
Kwa mujibu wa hilo jedwali, wanawake ni wengi kuliko wanaume, lakini upande wa asilimia unaonyesha idadi ndogo ya wanawake. Hilo kwako sio tatizo?
Nimesoma mkuu lakini hiyo asilimia unajua imekojotoleqa kutokana na idadi ipi? Hapo ndipo ninapoona kuwa bado hatuwezi kuhitimisha kuwa ni ubatili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…