JokaKuu
Platinum Member
- Jul 31, 2006
- 30,441
- 55,018
Unaulizwa swali unaruka ruka tuu, inaonekana huna uwezo wa kujibu wala uelewa wa siasa za dunia hii.
..hili swala ni COMPLEX.
..zipo nchi zinaweza kufaidika kwa kuwa na population kubwa.
..na ziko nchi haziwezi kufaidika kwa kuwa na population kubwa.
..China ambayo Raisi aliizungumzia kwa muda mrefu walikuwa na sera ya " ONE CHILD POLICY." maana yake ni kwamba idadi kubwa au ongezeko na watu lilikuwa likiwaathiri kiuchumi.
..Nchi kama Japan wanalalamika kwamba idadi kubwa ya wazee imekuwa ni mzigo kwa nchi kwasababu vijana waliopo they are not contributing that much kwa serekali ili iweze kuwahudumia wazee.
..Marekani wana population kubwa lakini wana tatizo kama la Wajapani lakini lina mazingira tofauti.
Wamarekani nao hawana idadi ya kutosha ya wachangiaji ktk social security fund na huduma nyingine za kijamii.
..Lakini tatizo la US haliko kwenye population as idadi ya watu bali liko kwenye aina ya ajira ambazo zinazalishwa nchini humu.
..Kwanza, hawana idadi ya kutosha ya waajiriwa wanaochangia kutunisha mfuko wao wa social security.
..Tatizo lingine ni kwamba uchumi wao unazalisha ajira ambazo wakati mwingine wananchi wao hawana ujizi nazo.
.. Halafu kuna ajira ambazo ziko wazi lakini wananchi wao hawazitaki, kwa mfano kazi za mashambani. Na hawazitaki kwasababu hazilipi a living wage.
..Nigeria ina idadi kubwa ya watu lakini vijana wake wanajaribu kila njia kutoroka kwenda Ulaya. Nigeria pia ndiyo yenye uchumi mkubwa Afrika.
..Kwa hoja ya idadi ya watu, faida na hasara zake, ni pana na inategemea mazingira ya nchi husika. Swali ni kama Tz tutafaidika kwa kuwa na idadi kubwa ya watu, au tunatakiwa tupunguze kuzaana?