Magufuri ulisahau kuwa mke mkorofi dawa yake ni kuoa wa pili si kumfukuza

Ni kweli kuwa Magufuli alikuwa katika kutekeleza wajibu wake kama waziri mwenye dhamana. Ila ni kweli pia kuwa ama amefanya kwa makusudi ili tuone jinsi nchi yetu ilivyotekwa na wenye malori au alifanya pasipokujua impact ya uamuzi alioutoa.

Iwe iwavyo kuwa amekurupuka au hakufanya utafiti wa kutosha mambo machache yanakuwa bayana:

Mosi! Ni kweli kuwa kutegemea malori kwa shghuli ya usafirishaji wa mizigo ni hatari kwa uchumi wa nchi kwani hakuna nchi duniani iliyowahi kutegemea usafirishaji wa mizigo kwa njia hiyo ikaendelea.

Pili ni wazi pia kuwa, kusafirisha mizigo mizito kwa njia ya barabara ni kuharibu kwa kiwango kikubwa miundombinu ya barabara jambo ambalo linagharimu sana walipakodi kwani barabara hizo zinajengwa kwa gharama kubwa tena kwa mikopo ambayo inalipwa na walipa kodi.

Tatu ni kweli kuwa, miundombinu ya reli ilihujumiwa kwa makusudi ya kuwapa ulaji wenye malori bila kuangalia adhari za usafirishaji wa malori kwa taifa kama hili letu.

Kwa kugoma tu kwa wenye malori tuliona jinsi bandari ilivyoadhirika pia. Hii ikiwa na maana kuwa wenye malori wakiamua sasa hivi kutokusafirisha mizigo toka bandarini basi bandari nayo inafugwa kwa kuwa tunategemea wenye malori kwa shughuli hiyo.

Kwa hili lililotokea kama nchi hii ina watu wenye uchungu na taifa hili, nategemea kuwa jambo la kipaumbele lingekuwa ni kufungua reli zetu haraka iwezekanavyo. Kwa maneno mengine kukosekana kwa usafiri wa reli kusafirisha mizigo hilo ni janga la Kitaifa.

Tutajenga barabara kwa mabilioni ya shilingi lakini baada ya mwaka mmoja tu zitakuwa zimeharibika.

Hii ni hatari kuliko tunavyoweza kuwaza.

Kweli kabisa Danisamweswa,ulilosema ni ukweli mtupu naungana nawe asilimia mia.Yaani ni janga la kitaifa kufikiri usafiri wa barabara utachukua nafasi ya usafiri wa reli na kukidhi haja zaidi ya usafiri wa reli,ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.Hatuwezi kukuza uchumi wetu kwa mtaji hou,RELI PEKEE ndiyo itakayotuvusha kwani ina uwezo maradufu wa kusafirisha mizigo mizito na kuishi miaka mingi(life span)kuliko barabara za lami ambazo zinajengwa kwa gharama kubwa sana.

Natambua urasimu,ufisadi na kutowajibika ndio cancer inayoitafuna nchi hii,lakini tuombe Mungu atakuja Raisi mithili ya Mwl.Nyerere,hakika naamini ufisadi huu wa wakubwa utafikia mwisho na tena kwa gharama kubwa kwao mafisadi wenyewe pamoja na familia zao.Historia hujirudia kumbuka enzi za Sokoine jinsi wahujumu uchumi walivyofanywa..........it is coming soon it's a matter of time.

Pamoja na utendaji kazi mzuri wa Magufuli,kwa hili amechemka aidha kwa kutojua outcome ya amri zake zisizopenda kushirikisha wadau hata kama zina ukweli ndani yake.Hili ndio tatizo kubwa la Mheshimiwa Magufuli UBABE,anapaswa ajirekebishe mapema kabla halijamharibia sana taswira yake kwa wadau wa sekta yake(ujenzi) na watanzania kwa ujumla.

Tatizo hili la UBABE bado ni tatizo kubwa miongoni mwa viongozi wengi hapa Tanzania,lakini sasa wanainchi wengi tumeanza kujua haki zetu za msingi katika kila jambo limnalohusu ustawi wa maisha yetu kwa ujumla. Na tuzidi kuelimishana kila inapobidi na tukatae watanzania kuburuzwa na kauli na amri za viongozi wetu hasa pale tunapoona hatutendewi haki,au kwa kutoshirikishwa mapema, kabla ya maamuzi mazito hayajatolewa dhidi yetu wenyewe au mali zetu.
 
ushauri uliompa ni wa kiukweli mno ! Lakini kwa bahati mbaya sana Magufuli haamini kama kuna mtanzania yeyote mwenye akili kama yeye au zaidi yake , siku zote huamini kwamba yeye ni bora zaidi , hana tofauti kubwa na Lowasa .
 
ushauri uliompa ni wa kiukweli mno ! Lakini kwa bahati mbaya sana Magufuli haamini kama kuna mtanzania yeyote mwenye akili kama yeye au zaidi yake , siku zote huamini kwamba yeye ni bora zaidi , hana tofauti kubwa na Lowasa .
Kwa sakata hili Magufuli kajitia kidole mwenyewe, na kwa upande mwingine wa shilingi ni habari nzuri sana kwa fisadi Lowasa.
 
Back
Top Bottom