Davion Delmonte Jr.
JF-Expert Member
- Oct 27, 2013
- 2,149
- 1,717
Hatua ulizozipiga mpaka sasa zimewapa wananchi walio wengi faraja na dalili za kuonekana neema siku zijazo. Kwa mwendo wa kasi unaoenda nao ilikuwa ndio wakati muafaka sasa kurejesha imani ya wananchi kwa kuongeza uhuru katika bunge ili wasaidie kutia pilipili yale majipu unayoyakamua ili wahanga waipate dezo yao.
Lakini muheshimiwa Rais sijui imekuwaje tena serikali yako inaanza kuwapa sababu wananchi na wakosoaji wako sababu za kuichukia na kuikosoa serikali yako kwa jambo dogo. Inakuwaje na kwanini serikali itake kuzuia vipindi vya bunge kwa sababu zisizokuwa za mashiko?
Mh. Rais mimi sitaki kumkosoa yule waziri wako kwani ni wazi kabisa suala hili lilijadiliwa kwenye vikao na mawaziri ambapo wewe ni mwenyekiti hapo. Kwa hiyo moja kwa moja kama jambo hili ambalo kwa namna moja linahodhi uhuru wa kupata habari kwa wakati lililotangazwa na waziri wako likitekelezeka, ina maana kwamba serikali yako itaanza kuonekana ni ya mabavu na kufunika hizi juhudi kubwa unazozifanya sasahivi za kutumbua majipu na kurejesha hadhi ya taifa letu.
Unajua jambo dogo ukishalitilia mkazo unalipa uzito usio stahili. Mimi binafsi huwa siangalii vipindi vya bunge na nina uhakika zaidi ya asilimia 80 ya watanzania hawafanyi hivo. ila kitendo cha serikali kuliibua hili suala kumetupa sisi asilimia zaidi ya 80 hoja za kuanza kuhoji ni kwanini lisioneshwe kwenye kideo? Unaona kabisa tayari taifa zima limetaharuki kwa jambo dogo kiasi hiki. Na tayari imeashaanza ku backfire huku mitaani maana wabunge wa chama chaka ambao wametetea hiyo issue ndogo tayari wananchi walio wengi wanaanza kuwananga.
Tafadhali mh. Rais usiruhusu hoja ndogo kama hizi zitie doa uongozi wako ambao unakolea moto sasa.