Magufuli tumbua Viongozi vyama vya kuweka na kukopa

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,902
51,994
Serikali imekuwa na nia ya kuwasaidia wananchi kupitia vyama vya kuweka na kukopa na kupitia vyama vya ushirika.Vyama hivi huangaliwa na maofisa ushirika kuanzia usajili ,ukaguzi nk

Tatizo lililoko kwenye vyama vya kuweka na kukopa ni kama ifuatavyo

1.Viongozi kujikopesha pesa.Hivyo pesa nyingi huishia kwa viongozi kujikopesha na kutofanya marejesho na hivyo kupelekea pesa kuishia kwa viongozi na wale wawapendao ambao huwakopesha na kutofanya marejesho.Nashauri viongozi wa ushirika wakague mikopo yote ya viongozi wa vyama vya kuweka na kukopa nchi zima waone maajabu.

2.Viongozi wa vyama kutoitisha mikutano ya wanachama na kuwasilisha ripoti za fedha.Viongozi mafisadi wa vyama hivyo vya kuweka na kukopa hawaitishi mikutano ya wanachama na maofisa ushirika huwa hata hawafuatilii kuhakikisha vyama hivyo vya kuweka na kukopa vinafanya mikutano kama inavyotakiwa.Hao maofisa ushirika nao wa kutumbua.

3.Viongozi wa vyama vya kuweka na kukopa kutoitisha chaguzi kulingana na katiba.

Nashauri Raisi atumbue huko kwa kuwa kabla ya kuanza kusambaza zile milioni 50 kila kijiji kunatakiwa kusafishwe na kutumbuliwa kwanza uongozi wa hivi vyama vya kuweka na kukopa vya mijini na vijijini na vile vya taasisi mbalimbali za umma na za binafsi.Kuna madudu ambayo si ya kutumbua tu bali viongozi wake wanatakiwa kufilisiwa hata mali zao kurudisha mapesa waliyojikopesa ambayo hawayarejeshi.

Kama kuna jipu liko kubwa vyama vya kuweka na kukopa pia.Maofisa ushirika wasaidiane na raisi kulitumbua hasa maeneo hayo niliyoainisha.
 
Ni kweli kuna changamoto hizo. Hata hivyo, nakushauri ujifunze zaidi kuhusu ushirika wa akiba na mikopo ili uangalie mamlaka zilizopewa jukumu la kufanya hivyo.
 
Ni kweli kuna changamoto hizo. Hata hivyo, nakushauri ujifunze zaidi kuhusu ushirika wa akiba na mikopo ili uangalie mamlaka zilizopewa jukumu la kufanya hivyo.

Kama zimeshindwa kufanya ndio maana tunamwambia Raisi ili atumbue kuanzia maofisa ushirika wa wilaya,mikoa hadi wizarani kwa kushindwa kazi.
 
mh.raisi mwenyewe sijui kama ana mpango na vyama vya ushirika kwani hata wakati anazitaha wizara zake sikuona popote pale ushirika ulipo,naona upo hewano hewani tu,kuna tume ya ushirika imeanzishwa,sijui kwa kweli kama ina bajeti ya kutosha kuzikabili changamoto mbalimbali za sekta hii,kwa kweli serikali ikitupia jicho sekta hii kwa weledi kama misri vile,hii nchi itasonga vizuri sana,ikiwezekana hii sekta iwe idara kamili serikalini,isiwe chini ya mkuu wa idara ya kilimo
 
Back
Top Bottom