Magufuli sio mfumo ila yupo kwenye mfumo

MGOGO27

JF-Expert Member
Jan 5, 2016
459
217
ndugu zangu nimeamua kuwahusisha kuhusu huu uzi wangu humu kutokana na kauli za wachambuzi wa siasa,wanasiasa na hata viongozi wenyewe wa vyama na serikali kuwa MFUMO WA TANZANIA ndo tatizo na sio RAISI(HATA AJE MALAIKA HATAWEZA KWA MFUMO HUU)

Tatizo la nchi ya Tanzania ni MFUMO WA SERIKALI YA CCM na JPM ni sehemu ya serikali hiyo zaidi ya miaka 20 sasa naona hataweza kufanya mambo kama matazamio ya Watanzania wengi kwasababu zifuatazo

1.Kazi machoni pa wanahabari,jamaa amekuwa anafanya kazi machoni mwa kamera na kazi hizo hazinamuendelezo mfano siku ya uhuru walikusanya matakataka na hakukuwa na magari ya kutosha kusomba na kwenda kuhifadhi sehemu husika,sasa nchi haiwezi kuendeshwa na HISIA BINAFSI

2.Weredi na kufata sheria
weredi wake huyu jamaa unanipa wasiwasi sana mfano siku ya uhuru walikusanya takataka na wakachoma sehemu nyingi sasa sijui alijua kukusanya taka ndo usafi wa mazingira na kuchoma sijui hakujua kama inachafua zaidi mazingira haswa HEWA?
Anafukuza watu kazi bila kujali sheria ya kazi na anasema wameiba hela watu fulani ila hatuoni hatua zaidi kama kuwapeleka mahakamani au kuwafirisi au kiwafanya warudishe hela za walipa kodi mengine mengi ila nadhani kwa haya machache bado yeye mwenyewe hajui njia ya kutoka nje ya huu mfumo
 
Nimesoma uzi wako mara tatu sijaelewa hoja yako ni nini? Ina maana yanayoendelea hapa huyaoni ama wewe ni mgeni hapa Yerusalemu.
 
Nimesoma uzi wako mara tatu sijaelewa hoja yako ni nini? Ina maana yanayoendelea hapa huyaoni ama wewe ni mgeni hapa Yerusalemu.
Sijakuelewa hata kidogo?jifafanue
 
Maana yangu ccm ni ile ileeee Magufuli hawezi badilisha nchi kwa mfumo wa ccm na hata aje rais wa aina gani akitoka ccm hakuna kitu
 
Back
Top Bottom