GODZILLA
JF-Expert Member
- Dec 26, 2014
- 5,914
- 10,585
Rais Magufuli ni Rais shupavu na mwenye kujiamini. Ni wazi na inaonekana, wala sio swala la kujadili.
Kwanza niseme tu, binafsi ninahusudu Kiongozi anayezungumza na kutenda kwa MAMLAKA. Rais asiyebabaishwa wala kutikiswa.
Hata akizungumza unayaona MAMLAKA yanatoka kwenye kinywa chake!
Kipindi cha nyuma tulikuwa na Rais goigoi sana. Mchovu na dhaifu (japo ana mazuri yake mengi).
Tulikuwa na Rais ambaye watu walimshika sharubu na kumchezea bila kuwajibishwa. Alikuwa mstahimilivu na mwenye stara zilizopindukia.
Najaribu kufuatilia uongozi wa Magufuli, naona anapata tabu sana kuendana na mfumo wenye watu legevu na wasio na maarifa.
Watendaji wengi wa serikali bado ni wachovu na hawajitambui. Anajaribu kuwaburuza kwa ukali lakini bado wamezubaa.
Bila kuwa na mifumo madhubuti itakayokuwa inajiendesha yenyewe kwa kuwashughulikia wababaishaji na kudhibiti utendaji dhaifu, bado tutaendelea kupiga maktaim.
Ndio maana wengine wameanza kuwa na mawazo ya kumfanya Magufuli kuwa mfalme wa kudumu, maana ni wazi wanaona hakuna anayeweza kujaza pengo la udhaifu wa mfumo isipokuwa Magufuli.
Nchi yenye mifumo dhaifu inahitaji Kiongozi shupavu, lakini bahati mbaya hawezi kudumu milele.
Ukiwa na mifumo madhubuti, huhitaji Rais mwenye maguvu mengi au mwenye sauti ya chuma ya kuwatisha watendaji wa serikali. Mifumo inajiendesha.
Ikiwa Rais Magufuli anaipenda kweli Tanzania, atawezesha upatikanaji wa Katiba yenye mifumo madhubuti itakayodhibiti ubabaishaji na ujanja ujanja.