Kwani
JF-Expert Member
- Jan 12, 2016
- 455
- 562
Tanzania ni nchi iliyobahatika kupata raisi kutoka kwa mungu kama anavyojinasibu,pia Tanzania ni nchi pekee yenye raisi anayoyatumia vyema maneno yake.
Watu wataishi kama MASHETANI:Raisi wetu mtukufu aliwahi kutoa kauli hiyo na mambo haya yanaanza kutokea,mtu anayeishi chini ya dola moja kumuuzia sukari kg1 kwa Tsh.4000 ni kutaka aishi kama shetani,unabii hapa umeonekana na mtakuja kuamini kuwa ni nabii 2020.
Wataisoma NAMBA:Raisi wetu mtukufu kwa hili halina ubishi watu wanaisoma namba mpaka wanapata makengeza,wengine wanaisoma kwa kujificha wanaogopa kukwambia kuwa na wenyewe wanaisoma hiyo namba hususani vijana wako wa buku saba.
HAWACHOMOKI:Mtukufu raisi ni kweli kabisa wale waliojifanya wajanja hawachomoki kabisa na kuwaonyesha wewe ni nabii wa kweli wamekiona katika sherehe zao za CHASO,kwenye mkutano wao KAHAMA,pia pini kali alilopigwa MBOWE mwanza bila ajizi Raisi wangu ukawaonyesha kuwa hata katiba haitawasaidia waendapo bungeni umewaba kibano cha mende kula sungura.
Raisi wetu mtukufu naona kila mtu atakutii sasa ili kujenga taifa kwani sasa ukituambia mbu kameza chura tunabidi tukubali.