Awali ya note sina bidi kumpongeza Rais Pombe John Magufuli kwa kazi nzuri na makini anayoifanya mpaka hivi sasa ya kutumbua majipu; kazi yake ni ngumu na anahitaji kila msaada kutoka kwa note tunaolitakia mema Taifa letu. Uteuzi wake wa makatibu wakuu na manaibu wao unastahili pongezi kwani umelenga kuwateua watu kufuatana na taaluma zao na ndio maana wakina Profesa Mchome na Susan Mlawi wamepelekwa wizarra ya sheria kwani hio ndio fani yao na wengine wengi ni hivyo hivyo!! Hata hivyo ingawa kuna makatibu wa zamani wengine wanaendelea na wizara zao na wengine kuachwa; nimestaajabu sana kuondolewa kwa katibu mkuu wa wizara ya Afya Dr. Mbando kwani huyu bwana alikuwa ni mfano wa watumishi waliokuwa wanajali wananchi na kuheshimu kazi yake; ni mtumishi wa serikali ambaye alikuwa ofisini kila siku alfajuli saa kumi na mbili. Nalisemea hili mimi mwenyewe kama shahidi wa jinsi alivyonihudumia kama mwananchi asiyenijua lakini alinijali na kusikiliza matatizo yangu. Huyu alikuwa mfano mzuri wa watumishi waliojitambua hivyo ingawa Magufuli kamuondoa lakini ni hazina ambayo nchi haiwezi kuipoteza. Nawasilisha.