Magufuli na Tanzania mpya

gwamaka aswile

Senior Member
Mar 26, 2015
186
106
MAGUFULI NA TANZANIA MPYA

Kwanza nipende kumpongeza Rais wa awamu ya Tano Mh Dkt John Joseph Pombe Magufuli pamoja na Makamu wa Rais Mh Samia Hassani Suluhu kwa ushindi walioupata kwenye uchaguzi uliofanyika Octoba 25,2015 kwani uchaguzi wa mwaka huu ulijaa ushindani sana na ahadi za kila aina.

pili ni wapongeze hata wale ambao hawakufanikiwa kushindi na ni wapongeze kwa kuonesha ukomavu wa demokrasia ya kweli ya kukubali matokeo kwa amani bila kusababisha vurugu ya aina yoyote ile ambayo ingeweza kuvuruga amani yetu.

Nichukue nafasi hii kumpongeza Mh Dkt Magufuli Rais wa awamu ya tano kitendo chake cha kuzuia safari za nche baada ya kwenda hazina kimesaidia wanafunzi walio wengi kupata mikopo kwa ajiri ya kuendelea na masomo yake kama alivyoahidi kwa watanzania wakati akiomba ridhaa kwa watanzania kuwa wanafunzi wote walioomba mikopo ni lazima wapewe mikopo na wakasome, ahadi yake imetimia kwa kiwango kikubwa ambapo asilimia ya wanafunzi ambao wameshapata mikopo ni 48,469 kati ya wanafunzi 70,000 ambayo ni idadi kubwa ukilinganisha namiaka ya nyuma.

Mh Dkt Magufuli kwa kazi ambayo ameifanya ndani ya wiki chache ambayo zimeonesha uhalali na ukweli wa kauli yake ya mabadiliko ya kweli ya hapa kazi tu kwani imesaidia watanzania wengi kupata huduma wanazostahili kwani kitendo cha kufanya ziara ya kushitukiza katika Hospitali ya Muhimbili kimesaidia kupunguza ugumu wa huduma ambazo watanzania wengi hasa wale wamaisha ya chini pamoja na kuhakikisha wafanyakazi pamoja na vifaa vya upimaji vinakuwepo na wagonjwa wanalala sehemu nzuri.

Mh Dkt Magufuli Rais wa awamu ya tano pia amezidi kuushangaza ulimwengu mzima kwa maamzi yake hususani kuzuia matumizi makubwa ya fedha katika mambo yasiyofaa mfano baada ya kupeleka jina la Waziri mkuu na kesho ya kwenda kufungua bunge baadae kulikuwa na sherehe ya wabunge ambayo ilikuwa inagharimu shilingi million 256 ambapo Mh Rais aliamuru fedha hizo zielekezwe katika huduma ya Afya hususani hospitali ya taifa kwenda kununua vitanda ilikupunguza shida wanazopata wagonjwa wanaolala chini wakiendelea na matibabu na kuwaamuru watumie milioni 10 au 15 tu.

Pamoja na hilo Rais anazidi pongezwa na watanzania wengi kwa kuhakikisha matumizi ya anasa yasiyo kuwa na faida kwa watanzania na Taifa kwa ujumla yasipate kipaumbele pia hatua hizo za Mh Rais zimepokelewa kwa furaha kubwa na watanzania wengi.

Watanzania wengi tunaimani na Rais Magufuli kwa utendaji wake wa kazi na tunaimani ataweza kulisaidia Taifa letu katika kuongeza uchumi na kuzuia mianya ya rushwa na ufisadi pamoja na uuzaji wa madawa ya kulevya.

Watanzania kama tunataka Mh Rais atimize hayo yatupasa kumuombea sana maana kazi hiyo siyo rahisi kama tunavyodhani wapo watu wanao taka kupambana naye iliashindwe kufanikisha dhana ya kuleta mabadiliko ya kweli.

Mwanafunzi wa Chuo cha Ustawi Wa Jamii
 
Ukiwa unaandika kitu kama unajua ni kirefu weka kwenye paragraph ili watu wa-pick points wanazotaka.
Mtu akisomga mistari mitatu akaona story inaanza kuboa au unaongelea kitu ambacho tushakizoea ataacha kusoma ila ingekua in paragraphs anasoma moja akiona imeanza kuboa ataanza nyingine.
 
ndugu Tanzania mpya yenye jamhuli ya muungano wa Tanganyika na Malawi au unamaanisha nn? Mm na walio wengi hatuoni hiyo Tanzania mpya.
 
ninyi mnaompa sifa jpm mapema hivi ndo walewale mtao mzomea mwisho wa siku...ukianza kwa kushangiliwa jiandae kumaliza kwa kuzomewa.
 
Tumeshuhudia raisi John Pombe Magufuri akichukua hatua mbali mbali katika kuijenga upya Tanzania. Uteuzi wake wa viongozi ktk nafasi mbalimbali unaonesha waziwazi anataka mabadiriko na maendeleo yapatikane hasa kwa mwananchi wa kawaida.

Naona ni wakati muhafaka sisi watanzania ndani na nje ya nchi kuunga mukono juhudi hizi. Kila mtu kwa nafasi yake awajibike kizalendo. Tupunguze blabla katika mambo yetu.

Kama umebahatika Kuwa na Kazi, basi ifanye kwa moyo na matunda yaonekane. Tupunguze kulalamika. Tufanyie kazi changamoto zetu tupunguze kutupiana lawama.

Binafsi naona tukijituma kila mtu kwa nafasi yake, hii nchi tutaijenga. Tumuombee pia raisi wetu na viongozi waamue kwa maslahi mapana ya nchi yetu. KWA PAMOJA TUTAFIKA.
 
Ila apunguze matusi na kashfa uchaguzi ulishaisha,chuki na visasi vya nini.Asituite tuliochagua upinzani watoto wa Mbwa,sisi ni binadamu tunastahili heshima
 
Ila apunguze matusi na kashfa uchaguzi ulishaisha,chuki na visasi vya nini.Asituite tuliochagua upinzani watoto wa Mbwa,sisi ni binadamu tunastahili heshima
Upinzani Ni afya kwa maendeleo. Kukubari kukisolewa Ni hekima. Tueleweshane tutafika
 
Upinzani Ni afya kwa maendeleo. Kukubari kukisolewa Ni hekima. Tueleweshane tutafika

Hili inabidi tulipigie kelele.Tuwaelimishe wanasiasa na wale wanachama wa vyama ambao wanaona kupingana kwa hoja haiwezekani mpaka tubaguane.
 
Back
Top Bottom