Davion Delmonte Jr.
JF-Expert Member
- Oct 27, 2013
- 2,149
- 1,717
Nimepita kwenye mitandao mbalimbali leo na nilichokiona ni kwamba "OIL" au "Mafuta" yameshuka sana na kufikia bei ya $32 kwa barrel moja ambayo ni ndogo zaidi kuwahi kutokea tangu mwaka 2003. Hii ni baada ya uchumi wa China kuendelea kuwa na mdororo na viashiria vya ku slow down kwa uchumi wa Marekani baada ya kupandisha riba ambayo kwa pamoja vimeshusha demand ya OIL na bei kuendelea kushuka huku mataifa ya OPEC yakiendelea kupump oil kwa wingi.
Baada ya kuona hili suala nilijaribu kufanya udadisi wa bei zilizopo kwenye masoko ya kitanzania lakini hali inatia huzuni. Hakuna kilichobadilika bei ni kama zile zile za 2000 zilizokuwepo zaidi ya mwaka mmoja uliopita ambapo yalikuwa kwenye soko la dunia yakiuzwa around $55-$60. Hakuna anayeongea chochote sio waziri husika, mamlaka husika wala chombo chochote kile kuhusu hili suala la mafuta.
Ni kama vile mafuta hayana umuhimu kwa taifa lakini sio kweli Tanzania kwa sasa inategemea umeme wa mafuta na bado wananchi wengi wanategemea mafuta katika shughuli zao za kiuchumi. Infact mimi sijaona kitu chochote ambacho kinaendesha maisha ya wananchi zaidi ya mafuta.
Lakini hali inasikitisha, inaonesha kwamba sekta hii yenye umuhimu kwa taifa bado inaendeshwa na ushawishi wa wafanyabiashara ambao naweza kusema ndo mpaka sasa wanasababisha tuendelee na bei hizi hizi kubwa za mafuta angali bei haipo hivo kwenye soko la dunia.
Ningependa rais na waziri husika wavalie njuga suala hili tena kwa dharura. Kama bei ya mafuta inashuka leo ina maana umeme utashuka bei kwa maana gharama za uzalishaji zitapungua, nauli zitapungua hivo ni nafuu kwa wananchi walio wengi, mfumuko wa bei wa bidhaa nyingine pia kwa namna moja utadhibitiwa, kwenye kilimo napo gharama za shughuli za kilimo kwa wenye matrekta pia zitapungua na hii inamaanisha uwezo wa kulima ekari nyingi za ardhi utaongezeka. Kuna faida nyingi nyingi sana za kuwa na unafuu wa mafuta ambao nikielezea tutakesha.
Kwa ufupi tu bei ya mafuta ikishuka ugumu wa maisha kwa namna moja ama nyingine utapungua. Na bei ndo kitu pekee ambacho kinaweza kusafiri kwa haraka kuliko kitu chochote katika mandhari ya uchumi. Yaani mfano ikatamkwa tu kwamba sasa mafuta yauzwe kwa 1500 ni kwamba mpaka kule Kantalamba au Nanyumbu watasikia na kesho yake watanunua mafuta kwa 1500.
Na ndio maana nchi nyingi zilizoendelea zina endelea maana masuala kama haya yanaamuliwa na "soko" ama "market forces" kama wanavosema wao ambapo bei inakuwa kwa haraka ina reflect forces za demand and supply kwa wakati huo. Sasa huku kwetu Tanzania sijui mfumo wetu wa uchumi upoje? Yaani bei kushuka mpaka watu wapigizane makelele na serikali akati ingetakiwa iwe automatic bei imeshuka kwenye soko la dunia na kwenye masoko yetu ishuke, sasa kinachozuia bei kushuka na kubakia kuwa juu kwa mda mrefu ni kitu gani? (hili ni jipu na litumbuliwe)
Najua watasema oooh tuna stock tulinunua kwa bei kubwa. Sasa ifaamike wazi na serikali ielewe kwa muda husika haya makampuni ya mafuta wamenunua hayo mafuta kwa bei gani. Maana kwa mwezi mmoja uliopita yalikuwa pia kwenye dola 40 na ingepaswa pia yawe chini. Hawa hawawezi kutudanganya eti huwa wanaagiza stock ya mda mrefu. Huu ni uongo wa wazi mi sidhani kama huwa inazidi hata interval ya wiki mbili kwa wakala anaeagiza mafuta vinginevo wataalamu walioko huko waje kutusaidia kwa hili.
Mi nasema imetosha mheshimiwa Rais na waziri husika hatuwezi tena kuweka rehani maslahi mazito na mapana ya taifa zima kwenye mikono ya wachache wafanyabiashara walafi. Hii ni issue nzito na ya dharura "bei ya mafuta ishuke kwa manufaa ya watanzania"
Kuna mambo umeyafanya mazuri mpaka sasa kama 1) Kubana matumizi ya serikali 2) Kupambana na mafisadi ndani ya taasisi za serikali na 3) Elimu bure naomba kwenye CV yako uongezee na hili suala zito la kushusha bei ya mafuta ambayo ndiyo pekee inayoweza kutugusa na sisi watu wa Nanyumbu maana hiyo bomomoa huko Dar sisi huku haitusaidii.