Magufuli na mafisadi, Duterte wa Phillipines na wauza unga

Ki Mun

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2014
Posts
3,442
Reaction score
4,393
Kuna mambo yanayoendelea huko nchini Phillipines kwa 'amri' za Rais mpya wa nchi hiyo Rodrigo 'Rody' Duertete yanafanana kiasi na ambayo yanatokea/au kuna dalili kuwa huenda yakatokea hapa kwetu, hasa wakati huu amabapo kile kinachoitwa "mahakama ya mafisadi" kinaenda kuanza chini ya utawala wa Rais Magufuli.

Duertete alishinda uchaguzi kwa ahadi ya kuhakikisha 'amewafutilia' mbali anaowaita 'wauza madawa' ya kulevya 100,000 nchini mwake. Hadi sasa watu 3000 'wamepotezwa' (kiholela). Marekani, Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa wanakosoa, raia wa Phillipines wanashangilia. Polisi wana leseni ya 'kumpoteza' yeyote anayehisiwa kuwa ni dealer na Rais anawaahidi hawatashtakiwa kwa kazi hiyo wanayoifanya. Lakini inaonekana wanaolengwa hasa ni wapinzani wa kisiasa wa Rais Duertete. Obama alipohoji aliitwa 'mwana wa kahaba' na Ban Ki Moon ameitwa 'a fool' na Rais huyu.

Hapa kwetu leo Jaji Mkuu ametangaza rasmi kuanza kazi kwa 'Mahakama ya Mafisadi'...ilikuwa ni ahadi ambayo pengine nayo ilimsaidia Rais Magufuli kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka jana. Rai yangu ni kuwa mahakama hii ijiepushe kutenda yale yanayotendeka Phillipines. Watu wasibambikizwe ufisadi na mashtaka wasiyohusika nayo - labda kwa sababu tu ya kuonekana wanamkosoa Rais na chama chake.

Hata hivyo nahofu kuwa Mahakama ya Mafisadi ya Tanganyika itaibua taharuki sawa na taharuki ya kile kinachoendelea Phillipines, na ni watu wa upande mmoja tu ndo huenda wakaguswa na kesi hizi - kamwe simwoni Rais Magufuli akiridhia makada wa chama chake washtakiwe katika mahakama hii. Ikiwa hivi, nchi yetu itavurugika, na hasa ikizingatiwa kuwa ni raia wa Tanzania Bara tu ndo watakuwa wakishtakiwa katika mahakama hii - isije ikatokea kuwa kesi kama zile za Mbowe Hotels vs NHC zikatengenezwa kuwa kesi za kifisadi;tukifikia hapo tutaivuruga nchi yetu.
 
Ianze na ESCROW maana nasikia kulifanyika utapeli / wizi as a result tunadaiwa tena
 
Usiwapotoshe watu wewe, Rodrigo Duterte (anaglia Jina lake linavyoandikwa), kabla ya kuwa Rais, alikuwa meya wa mji wa Davao city, moja ya miji hatari sana nchini Philippines na duniani kabla ya Duterte kuwa meya. Yeye aliweza kusafisha na kuondoa uchfu wote katika mji huo na sasa kuwa Davao city ni moja ya miji salama sana duniani, na hiyo ndiyo sababu kubwa sana ya yeye kuchaguliwa kuwa Rais wa Philippines maana nchi hiyo imejaa uhalifu wa kila aina na madawa ya kulevya, na yeye aliwaahidi wananchi wake kuwa wakimchagua basi ataondoa uchafu wote huo kama alivyofanya huko Davao city (uki google utaona yote hayo), hakuna ukweli wowote ule kuwa anawamaliza wapinzani wake, ila ni kweli ma drugs dealers anawaua (siyo TZ bado wanakumbatiwa), na haya ni maneno yake:
“We will not stop until the last drug lord … and the last pusher have surrendered or are put either behind bars or below the ground, if they so wish,” said Duterte.

Hivi mnajua hizo crimes zilizopo huko Philippines? ndiyo maana wananchi wamemchagua ili amalize hilo tatizo, sasa mpeni mwaka mmoja tu halafu mtasikia philippines iko wapi. Hao wanaojiita vinara wa demokrasia wanaomlaumu na kumbeza ni wanafiki wakubwa, hawataki kuona nchi zetu zinaendelea mbele na kuwa huru, ila wao wakifanya hivyo basi ni sawa tu.
 
Back
Top Bottom