Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,405
- 23,581
Kwa CCM nachoka...! Flashback...30/9/2015

Amesema kupitia safari hizo, Rais Kikwete amefanikiwa kuwashawishi wafadhili kutoa misaada ya miradi mbalimbali nchini.
Aliyasema hayo kwenye mkutano wa kampeni katika kata ya Mvumi Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma jana.
Dk. Magufuli alitoa mfano wa Sh. bilioni 992 zilizotolewa na Serikali ya Marekani hivi karibuni kupitia mfuko wa MCC kwa ajili ya miradi ya umeme kama sehemu ya matunda ya safari za Rais Kikwete nchi za nje.
Fast Forward...27/3/2016

Rais Magufuli ametoa wito katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Azania Front Jijini Dar es salaam, ambako amesali ibada ya Pasaka pamoja na waumini wa kanisa hilo.
Rais Magufuli amesema tukifanya kazi hatuhitaji hata misaada kutoka nje, nchi hii ina neema nyingi.
Katika kusisitiza amesema tukifanya kazi kwa bidi nchi yetu inapaswa kuwa inatoa misaada kwa nchi nyingine na sio kuomba misaada kutoka nchi nyingine.
Hii imekuja baada ya Marekani kusitisha msaada wake kupitia mfuko wa MCC kwa ajili ya miradi ya umeme aliodai awali kama sehemu ya matunda ya safari za Rais Kikwete nchi za nje