Magufuli kuzindua ndege mpya za ATCL trh 28/9/2016

Magufuli kuzindua ndege mpya za ATCL trh 28/9/2016

Mr Hero

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2015
Posts
5,540
Reaction score
7,464
Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli kesho anatarajiwa kuzindua ndege mbili mpya aina ya Bombardier Q 400 zilizonunuliwa na Serikali hivi karibuni.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) Dk Leornard Chamuriho amesema maandalizi yote kwa ajili ya uzinduzi wa ndege hizo yamekamilika na uzinduzi huo utafanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kuanzia saa mbili asubuhi.

“Tunawaomba wanahabari na wananchi kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi huo ili waone utekelezaji wa ahadi wa Serikali katika mkakati wa kuhuisha usafiri wa Anga hapa nchini”, amesema Dk Chamuriho.

Ndege hizo aina ya Bombardier Q 400 zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja zimetengenezwa nchini Canada na zitahudumia soko la ndani ndani na nchi za jirani zitakapoanza kazi.


Chanzo: Mwananchi



 
kwani zile ni mpya au zimepitwa na wakati?

Wabongo bana ukiwabana watakwambia zile ni ORIGINAL na wala si mtumba au special !..
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli kesho anatarajiwa kuzindua ndege mbili mpya aina ya Bombardier Q 400 zilizonunuliwa na Serikali hivi karibuni.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) Dk Leornard Chamuriho amesema maandalizi yote kwa ajili ya uzinduzi wa ndege hizo yamekamilika na uzinduzi huo utafanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kuanzia saa mbili asubuhi.
http://www.mwananchi.co.tz/…/1597578-3396390-43j…/index.html
Viva Ngosha
Vipi tutapanda bure kama mwendo kasi
 
Ni vizuri tuwekeeni nauli za chini ili na sisi mashetani angalau mara moja moja tupande. Ikiwa 30,000 mpaka 70,000 tutajitosa lakini zaidi ya hapo ni malaika tu ndio watafaidi
 
VIVA VIVA VIVA JPM - Tunafanya Tanzania kuwa kama Ujerumani (bidhaa za viwanda lazima zingine zisafirishwe kwa ndege).
Hapa CDM mpaka wanahisi kupasuka!
CCM CCM CCM CCM CCM!
 
Jamaa hana aibu kabisa anazinduwa mitumba ndege za mapanga dunia ya leo nadhani watakao shangaa ni watu wa chato
 
aisee nimekosa kuona JPM anavyomwenya kwa furaha kuirudisha tanzania ya ndege
 
Hahahaha Nimeipenda hii maana alisema tutaishi kama mashetani! Sasa sijui sisi mashetani tutaweza kupand hizo ndege za malaika!
Ni vizuri tuwekeeni nauli za chini ili na sisi mashetani angalau mara moja moja tupande. Ikiwa 30,000 mpaka 70,000 tutajitosa lakini zaidi ya hapo ni malaika tu ndio watafaidi
 
Ni vizuri tuwekeeni nauli za chini ili na sisi mashetani angalau mara moja moja tupande. Ikiwa 30,000 mpaka 70,000 tutajitosa lakini zaidi ya hapo ni malaika tu ndio watafaidi
***
KAZI YA SUMATRA...!
 
Back
Top Bottom