Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,042
- 10,787
Leo Mtukufu wa nchi mkuu sana Rais Magufuli wakati akiwaapisha wakuu wa Mikoa wapya na wakuu wa wilaya kula kiapo cha uadilifu alitamka ''Tulikuwa tunafuatilia kwenye revenue, yuko mtu mmoja alikuwa anafanya transaction ya fedha kila dk 1 kati ya milioni 7 na 8. Serikali ilikuwa inapoteza pesa, bahati nzuri huyo mtu yuko mikono salama, tunatafuta jinsi ya kuzirudisha''
“Tulikuwa tunafuatilia kwenye ‘revenue’ (mapato), kwenye zile VAT ambazo zinatumika ‘ku-collect revenue’ (kukusanya mapato), yupo mtu mmoja ambaye alikuwa ametengeneza kampuni zake nyingi, alikuwa anafanya ‘transaction’ (miamala) ya fedha kila dakika moja kati ya Sh milioni saba na nane.
“Na hizo risiti alikuwa anaziuza kwa wafanyabiashara wengine, kwenye VAT anatakiwa kulipia kwa asilimia 18. Wafanyabiashara wengine hao walikuwa wanauziwa kwa asilimia tano na wakishauza bidhaa wanakwenda kuomba TRA iwarudishie hiyo asilimia 18, kwa hiyo Serikali imekuwa ikipoteza asilimia 18.5, ni matrilioni na matrilioni ‘of money’ (ya fedha).
“Bahati nzuri huyo mtu yuko kwenye mikono salama, tunafuatilia namna tutakavyorudisha hizo fedha, na huyo mtu alikuwa ana-connection kati ya watu wa BRELA na TRA… hiyo ndiyo Tanzania.
“Najaribu tu kutoa mfano ili katika maeneo yenu mkasimamie mapato ya Serikali, kwa sababu tumepoteza mapato mengi kuliko tunavyofikiria, huku Watanzania wakiteseka sana, na mambo yanayofanyika ni ya ajabu,” alisema Rais Magufuli akiwaambia wakuu hao wa mikoa na wilaya.
Kauli hii imeniacha njia panda, kwamba huyu mtu

- Alipata wapi ujasiri wa kuhamisha kiashi hicho cha fedha kila baada ya dakika moja?
- Hizo fedha zilikuwa kwa wema au ubaya?
- Huyo mtu ni nani mpaka asitajwe wananchi wakamjua?
- Yuko mikono salama, Hiyo mikono salama ni ipi kwa mtu wa namna hii?
- Watazirudisha vipi pesa zote alizohamisha?
- Amekuwa akihamisha pesa kwa muda gani na mpaka anawekwa mikono salama alikuwa kashachukua kiasi gani?
- Atapelekwa mahakama ya uhujumu/mafisadi?