Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 14,176
- 25,919
Ni habari iliyoenea sana katika ngazi za juu, kwamba kufanikiwa kwa Magufuli kupeperusha bendera ya CCM kwenye kugombea raisi nguvu kubwa nyuma yake ni Raisi mstaafu Benjamin Mkapa. Kuna sababu kadhaa zinazotolewa, na jinsi Mkapa alivyofanya kufanikisha hili.
La kwanza inasemwa Mkapa ilibidi amshawishi JK kwamba Magufuli kuwa raisi ajaye ni kwa faida yao wote, kwamba mojawapo ni Magufuli pekee ambaye watakuwa na uhakika wa asilimia 100% kwamba atawalinda kutokana na lolote ambalo wanaweza kusakamwa nalo (mfano suala la Kiwira, nk nk). Kulikuwa na suala la athari ya yale Magufuli aliyofanya, mfano kuhusiana na uuzaji wa nyumba za serikali - kutia ndani na kumuuzia ndugu yake - lakini ilionwa kwamba hilo si jambo kubwa, hasa ukizingatia kwamba pamoja na hayo bado Magufuli alikuwa ana mashabiki wengi katika watu wa kawaida.
Pia ilionekana wazi kwamba JK hakuwa na mtu chaguo lake ambaye aidha alikubalika kwa watu na angeweza kufanya kazi kwa maslahi ya maraisi waliopita - kutia ndani kuwasikiliza. Hatimaye makubaliano yalifikiwa, kwamba na iwe Magufuli. Magufuli aliambiwa juu ya hili, na hata kushauriwa namna ya kujitokeza kuwa mgombea - kimya kimya kabisa.
Lakini sasa, tutarajie kiasi gani cha influence ya Mkapa au JK kwa maamuzi ya Magufuli akiwa raisi? Inasemwa kwamba Magufuli ni mtu wa Mkapa 100%, na sio vibaya kutarajia chochote Mkapa atakachosema Magufuli atafanya, akijua wazi bila Mkapa yeye Magufuli asingekuwa alipo leo. Influence ya JK kwa Magufuli ni kidogo sana, na hata ile kidogo lazima iwe na baraka za Mkapa.
Kwa nini Mkapa awe na influence kiasi hicho kwa Magufuli? Inasemwa kwamba influence hiyo inatokana na urafiki wao binafsi. Wengine wanadai Magufuli alikuwa kwenye "system", yaani intelijensia ya Mkapa na serikali kabla hata hajawa Mbunge na kuteuliwa Waziri Mdogo, toka enzi Magufuli akiwa mwalimu.
Lakini watu wanaomfahamu wanamuonaje Magufuli kama Raisi? Wengi wanaona Tanzania ilipofikia inahitaji raisi kama Magufuli - namna fulani ya bulldozer ambalo linatumia nguvu bila kuangalia lojiki. Hata hivyo, wengi wana wasiwasi sana na influence ya Mkapa kwa Magufuli - kwamba itakuwa kama Makapa karudi kwenye uraisi, na wengi hilo hawalitaki.
Na wengine wana wasiwasi sana juu ya silka ya Magufuli katika kufanya maamuzi, wakisema ingekuwa Magufuli ndiye raisi kipindi cha JK, Tanzania ingekuwa imeshapigana vita na Rwanda na Malawi. Kuna wengine wanakumbusha jinsi Magufuli alivyokataa bila kushaurika kusafirishwa kwa boat za Azam kwenda Ziwa Victoria, ikabidi Mwandosya awaombe Kenya zile boti ziende ziwa Victoria kupitia barabara za Kenya. Na wengine wanakumbusha jinsi alivyokataa mabasi ya Zambia kupita barabara ya Tanzania Zambia, wakakwaruzana na Mwakyembe. Wengine wanadai ana silka ya kulipiza kisasi. Kuna mtu aligusia kwamba anaweza kukusweka ndani kwa sababu binafsi (eti alishaweka mume wa mtu ndani kwa sababu za ugomvi wa kimapenzi)
Vipi kuhusu mitandao kama JF? Kuna wengine hata wanasema katika uraisi wa Magufuli, uhai wa Mitandao ya Jamii kama JF uko mashakani sana!
Lakini kwa ujumla, watu wanasema huenda ni wakati muafaka kwa Tanzania kuwa na raisi kama Magufuli. Nchi imeharibika sana.