Magufuli hata kama anatamani kuwa dhalimu,katu hatawafikia Kagame na Museveni.

Ki Mun

JF-Expert Member
Oct 6, 2014
3,443
4,386
Nasema hatawafikia hao nikiwa simaanishi kwamba hataweza kutesa raia wa nchi yake mwenyewe kama hao, bali nafikiri tu kuwa hana maarifa wala umahiri wa kucheza na siasa za kitaifa na kimataifa kama hao. Kwa hiyo ni heri tu angeachana na fikra za kutawala kama Kagame na Museveni, kwa sababu atakapokuja kubanwa tokea pande zote,hatamudu kujinasua kama ambavyo Kagame na Museveni wamekuwa wakijinasua kutoka skendo mbalimbali za kuongoza nchi zao vibaya(kwanza Magufuli akumbuke wenzake Kiingereza wanakiongea kwa ufasaha kwa hiyo uwezo wao wa kuwasiliana kitaifa na kimataifa ni mkubwa mno)

Kwa hiyo rai yangu, Magufuli awaache Zitto na Mbowe wafanye kazi zao za kisiasa, kwa sababu akiendelea kuwasumbua watamgeuza kuwa kichekesho kabla hata hajamaliza mwaka katika 'uongozi' wake!

 
Back
Top Bottom