Magufuli fukuza watumishi wote. Ajiri upya na kuweka KPI kama staff wa Big 4 proffessional firms

we unatolea mfano ubalozi wa marekani!! electrician ambaye amesoma veta trade test pale ubalozini analipwa 1.2mil per month na bado kuna benefits kibao anapata. Electrician huyo huyo na hizo qualifications serikali yako ya magu analipwa 380000 per month. Alafu unakuja kuongea blah blah hapa, unafikiri ukiwa bosi kazi yako ni kuwaambia watu hapa kazi tu. Kazi hiyo bila motivation nani atafanya.
 
Najua wengi watachukia, ila ili hii nchi iendeleee lazima watu tufanye kazi. Navyosema kazi namaanisha kazi hasa, kila mtu awe busy kama staff wa kpmg, delloite, pwc, ey.. etc...

Sijawai ona staff wa oil and gas company kama petrobrass au halliburton ana muda wa kuuzulia hata birthday parties, ila watumishi wa umma wana muda huo wengi tu.

Hawana targets kazi wanafanya kwa spidi ya kobe. Nilikuwaga mtumishi wa uma zamani kabla sijasepa. Maana ofisi watu wamekalia wanawaza posho, semina na majungu tu.

Niko upande wa magufuli, kuongeza mshahara kwa watu wasiozalisha sio sahihi, Japo watasema utumishi wa uma ni huduma. Wafike ubalozi wa marekani waone watumishi wa uma wa serikali ya marekani aka department of state walivyo busy. Hata simu zao binafsi hawazitumii wakiwa kaziniii.

Ili viwanda vije lazima tuige utamaduni wa walioendela au huawei kwa mafano.. ni kampuni ya serikali ya china.. fika pale jubelee tower posta.. uone staffs wa huawei wachina walivyo busy muds wa kazi

Hivi kwa nini watu ambao hawajawahi kutoka nje ya nchi wana ndoto za alinacha hivi? Huko serikalini kwenye spidi ya kobe ni wapi? maana kama unazungumzia halmashauri hata marekani ni hivyo hivyo.

Umewahi kufanya kazi kwenye taasisi kama Benki Kuu, Ikulu, Idara ya Usalama, Ofisi ya waziri mkuu, TPDC na EWURA? Jaribu uone mchakamchaka wake, hizo big four ni cha mtoto. Unaweza kupigiwa saa sita usiku na kupewa maagizo ya kazi, na unaweza pia kuambiwa kuna safari jioni wakati ni saa sita mchana, unaweza kutakiwa kutoa taarifa inayokuhitaji kutumia ujuzi wa ICT, Mafuta na gesi, Fedha na uchumi, Ulinzi na Usalama, Media Scanning, sheria n.k ndani ya kipindi kifupi na bila mjadala na bado hapo wewe ni sawa na ngazi ya Associate aliyeko PWC au KPMG au Deloitte.

Suala la watanzania kuwa slow ni kote hata huko big four unakosema, ufanyaji kazi wa watanzania PWC hasa wa ngazi za Associates ni slow sana ukilinganisha na Associate aliyeko London. Hilo ni suala la nchi nzima sio serikalini tu.

Ni suala la mfumo uliokupa malezi tangu ukiwa mtoto, yaani je ulilelewa kuona kazi kama kitu chema au ulilelewa kuona kazi kama adhabu!??

Usidhani kujua tu Big Four, sijui Ubalozi na upuuzi gani ndio kujua kila kitu. Hayo ni mawazo ya ki-'Tanzanian Undergraduate'.
 
Ili swala nilishawahi lifikiria siku nyingi mno. Nadhani ajira zikiwa za mkataba zitaondosha ile hali ya waajiriwa kubweteka na kuanza kutengeneza network za kifisadi. Watu waangaliwe jinsi gani wapo active ku deliver na kufikisha goals za mwaka mzima. Isiwe watu wanaenda kazini tu kama wajibu halafu output ni 0% hasara tupu.

Nakubali kwamba waajiriwa wengi ni wazembe lakini vilevile ukumbuke kwamba waajiri wengi pia ni mafisadi ukiwemo ufisadi wa kudhulumu haki za wafanyakazi. Sheria ya kazi inawabana wote waajiri wakorofi na wafanyakazi wazembe.

Sheria hii ikifuatwa vizuri hakutakuw ana mwajiri mkorofi na mfanyakazi mzembe. Taabu ni kwamba uzembe wa mfanyakazi unafidiwa na mwajiri kuwa mkorofi, yaani ni tradeoff au biashara fulani ya uhalifu wanaifanya.

Ndiyo maana mfanyakazi akianza kudai madai tena ya haki waajiri wanamtafutia angle ya kumfukuza na wanampata, kwa sababu ni kama vile haiwezekani mtanzania kutokuwa mzembe kazini.

Acha uzembe, acha wizi na hapo ndipo utaweza kusimama wima na kumkabili employer, na wapo wanaoweza hilo.
 
Section 15(1)(c) of Employment and Labour Relation Act, No. 6 of 2004 (ELRA) inasema kila mwajiriwa lazima awe na “Job Description”. Hakuna section inayosema kila mwajiriwa lazima awe na “KPI”.

Section 15(1)(c) of ELRA inasema mwajiri hawezi kukubadilishia “Job Description” bila wewe kuiridhia. Analazimika kwanza akuletee na wewe ujadili cha kuondoa au kuongeza kisha mnaikubali wote. Hivyo, unapokuwa na “KPI” mwajiri hapaswi kuileta kwa jinis anavyotaka bali lazima aombe ruhusa ya mwajiriwa ili aikubali hiyo “KPI” maana kwa uzoefu ni kwamba “KPI” ni kiwango tu cha kazi zilizoorodheshwa kwenye “Job Description” na sin je ya hapo.

Ukija kwenye kanuni za sheria hizi ziko zinaitwa “Employment and Labour relations (Code of Good Practice) Rules, 2007”. Kifungu cha 17(2) kinasema “Although the employer has the managerial prerogative to set performance standards, the standards shall not be unreasonable”.

Hivyo, usidhani kwamba eti bosi wako anaweza tu kujitungia kwamba leo nesi umehudumia wagonjwa 20 sasa mimi kama bosi wako nakupangia “KPI” ya kuhudumia wagonjwa 40! Hapa ukimfukuza kazi mtu kwa underperformance kama mnavyotaka, inabid wewe mwajiri ukathibitisha mahakamani kwamba kumpangia wagonjwa 40 ilikuwa reasonable. Hapa ndipo waajiri karibu wote nchini wamekuwa wakishindwa kwenye kesi hizi za “KPI”.

Hao mnaowataja kwamba wamefaulu zoezi la “KPI” si kweli kwamba wamefaulu. Kinachotokea ni kwamba wanalipa mishahara mikubwa wafanyakazi wao kisai kwamba wafanyakazi wenyewe wanajitesa kukaa hata usiku kufanya kazi ili wamalize kazi wapate hela nyingi. Lakini akiibuka mfanyakazi wa huko akawashitaki anaweza kuwashinda kesi kirahisi kwa kigezo kilekile cha “reasobability”.

Natumaini mmenielewa mnaopinga na mnaopenda “KPI” iwekwe serikalini. Namalizia tena, kikubwa kazini ni "Job Description" ambayo naamini hata mliomo humu, asilimia zaidi ya 90 hamna "Job Description" hapo kazini kwenu.

Hii ndo inaitwa Great think....to be logical Criticall,analytical coherent...
Ngoja nikuulize swali....je na ile ya kupangiwa any other duties BY YOUR SUPERIOR ...ambapo ipo kwenye job description haiwezi kuingia kwenye KPI?

Kama umenisoma vizuri ni kwamba nilikosea provision mwanzoni sasa nairekebisha kwamba Section 15(4) of ELRA inambana employer asikupe "job description" ambayo hukubaliani nayo.

Hivyo, kama "job description" ina maneno "and any other duties assigned by your supervisor" basi kwa mujibu wa hii Section 15(4) of ELRA ni kwamba wewe ulikubaliana na hayo maneno na umemruhusu employer akupangie kazi zingine tofauti na zile zilizomo kwenye "job description".

Kisheria ni kwamba kila neno lililomo kwenye "job description" umelikubali baada ya majadiliano yaani "consultation".

Sasa tatizo lenu nyinyi watanzania wengi ni kwamba mnaisakama serikali eti inaingia kijinga mikataba mibovu wakati kutokuwa na "job description" ni ujinga kuliko hata wa serikali, na pia ukiwa na "job description" inasema "and any other duties" huo tayari ni mkataba mbovu.

Kinachotakiwa ni kwamba tumia haki yako iliyomo kwenye Section 15(4) of ELRA ili kukataa uozo wowote kwenye "job description" au "KPI" na ikibidi mfikishane mahakamani kama employer analeta za kuleta. Mkiogopaogopa mtatawaliw ana Rais dikteta lakini vilevile mtatawaliwa na employers wakorofi.

Ninainukuu hapa hiyo Section 15(4) of ELRA inayosema hivi:

"Where any matter stipulated in subsection (1) changes, the employer shall, in consultation with the employee, revise the written particulars to reflect the change and notify the employee of the change in writing".

Ni suala la mfumo uliokupa malezi tangu ukiwa mtoto, yaani je ulilelewa kuona kazi kama kitu chema au ulilelewa kuona kazi kama adhabu!??
 
Najua wengi watachukia, ila ili hii nchi iendeleee lazima watu tufanye kazi. Navyosema kazi namaanisha kazi hasa, kila mtu awe busy kama staff wa kpmg, delloite, pwc, ey.. etc...

Sijawai ona staff wa oil and gas company kama petrobrass au halliburton ana muda wa kuuzulia hata birthday parties, ila watumishi wa umma wana muda huo wengi tu.

Hawana targets kazi wanafanya kwa spidi ya kobe. Nilikuwaga mtumishi wa uma zamani kabla sijasepa. Maana ofisi watu wamekalia wanawaza posho, semina na majungu tu.

Niko upande wa magufuli, kuongeza mshahara kwa watu wasiozalisha sio sahihi, Japo watasema utumishi wa uma ni huduma. Wafike ubalozi wa marekani waone watumishi wa uma wa serikali ya marekani aka department of state walivyo busy. Hata simu zao binafsi hawazitumii wakiwa kaziniii.

Ili viwanda vije lazima tuige utamaduni wa walioendela au huawei kwa mafano.. ni kampuni ya serikali ya china.. fika pale jubelee tower posta.. uone staffs wa huawei wachina walivyo busy muds wa kazi
akili ndogo
 
Mnapotaka kuandika mambo ya maana tulizeni akili ili muandike vizuri. Watumishi wa Serikali wanatoa huduma. Hawazalishi kama wa kiwanda cha vifaranga cha Amadori, au kiwanda cha chuma pale Mikocheni. Unaposema huwezi kuwaongeza watumishi mishahara kwa sababu ya uzalishaji, you need to know exactly what you are talking about. Mtu yeyote anayesema watanzania hawafanyi kazi ni mpuuzi sana. Completely disconnected with reality. Watanzania wanafanya kazi sana. Tena wanafanya kazi katika mazingira magumu kweli. Mfikirie babu yako aliyeko kijijini ambaye anakwenda shamba saa 10 alfajiri na kurudi saa 7 mchana na bado anapata gunia mbili tu za mahindi! Tatizo letu hapa, tunapojadili issue ya watu kufanya kazi, tunamwondoa mdau muhimu yaani serikali. Kama serikali haiweki mazingira ya kuwawezesha wakulima au wafanyakazi kufanya kazi zao kwa tija, huwezi kutegemea uzalishaji au tija. Mazingira ya kazi mazuri kwa wafanyakazi ni pamoja na mishahara inayowawezesha kuwa na utulivu na morali ya kufanya kazi. Wewe unampa mtu mshahara wa kumtosha kutumia wiki moja kisha unamtarajia atoe tija kwa mwezi mzima? Au hamjui frustration, stress, na disappointments zina madhara gani katika kazi??? Let's leap what we deserve.
 
hujui hata maana ya KPI.. kweli Tanzania ya viwanda ije inahitaji zaidi ya udikteta..

na hapo inaweza kuwa ni mkurugenzi wa halmashauri wewe ila hujui hata KPI ni nini.. ha ha ha
Katika uandishi wowote wa habari, lazima kichwa cha habari kije kielezwe ndani ya habari aidha mwanzo au mwisho wa habari. Sasa andiko lake ndani hakuna kichwa chake cha habari. Hebu changanua aliwezaje kufikia uamuzi wa kuchagua kichwa hicho cha habari? Tafadhali hizi shule zitusaidie kuelewa sio kupata credits nzuri tu darasani
 
Najua wengi watachukia, ila ili hii nchi iendeleee lazima watu tufanye kazi. Navyosema kazi namaanisha kazi hasa, kila mtu awe busy kama staff wa kpmg, delloite, pwc, ey.. etc...

Sijawai ona staff wa oil and gas company kama petrobrass au halliburton ana muda wa kuuzulia hata birthday parties, ila watumishi wa umma wana muda huo wengi tu.

Hawana targets kazi wanafanya kwa spidi ya kobe. Nilikuwaga mtumishi wa uma zamani kabla sijasepa. Maana ofisi watu wamekalia wanawaza posho, semina na majungu tu.

Niko upande wa magufuli, kuongeza mshahara kwa watu wasiozalisha sio sahihi, Japo watasema utumishi wa uma ni huduma. Wafike ubalozi wa marekani waone watumishi wa uma wa serikali ya marekani aka department of state walivyo busy. Hata simu zao binafsi hawazitumii wakiwa kaziniii.

Ili viwanda vije lazima tuige utamaduni wa walioendela au huawei kwa mafano.. ni kampuni ya serikali ya china.. fika pale jubelee tower posta.. uone staffs wa huawei wachina walivyo busy muds wa kazi
I partly agree with you partly not. for an employee to deliver, you need to show him/her a certain degree of respect, I know this is difficult because many of our leaders whom I have met do not have such sense of human respect; they go barking like dogs. In such an environment, do not expect your subordinate to deliver to the required standards. Give them some cakes where necessary apply a stick. By stick I do not mean to flog them, but reprimands. Appreciate good performances, where applicable reward them.
 
mkuu,kuna mifumo mingi ya kufanya kazi,kwa watumishi wengi wa umma mfumo wa kupima uko kwenye OPRAS.
hapo ndipo watu hupeana majukumu na pia njia ya kupima km yamefanikiwa na rasilimali zinazohitajika kufanikisha.
mfano kiutaratibu unapaswa uhukumu kesi 600 kwa mwaka au uende doria 600 kwa mwaka au upime viwanja 800 kwa mwaka au uhudumie wateja 200,000 kwa mwaka au ukague shule 600 kwa mwaka au unyonge watu 50 kwa mwaka au utetee kesi 700 kwa mwaka.sehemu ya mahitaji ni usafiri au rasilimaliu pesa au silaha au risasi au madawa au uwepo wa wafungwa wa kunyongwa.kati mahitaji yakapungua mfano unataka ninyonge watu 50 kwa mwaka ila waliohukumiwa wako 20.nikague shule mia nne na tumekubaliana unanipa usafiri na mafuta,umenipa mafuta ya kukagua shule mia au gari lipo mafuta hakuna.doria umenipa mafuta doria 200 ntaendaje mia sita.kesi zipo mikoani na mm ni wakili wa serikali ntaendaje wilayani sita kwa nauli ya nani na ww umenipa nauli ya wilaya moja.
 
Back
Top Bottom