Magufuli fukuza watumishi wote. Ajiri upya na kuweka KPI kama staff wa Big 4 proffessional firms

Ili viwanda vije lazima tuige utamaduni wa walioendela..

Hapa ndo huwa mnajichanganya....utamaduni wa waliondelea unajumuisha pia kuheshimu mawazo ya wengine na kuheshimu demokrasia, na kubishana na unaotofautiana nao kimawazo kwa hoja siyo bunduki, ebo!
 
Najua wengi watachukia, ila ili hii nchi iendeleee lazima watu tufanye kazi. Navyosema kazi namaanisha kazi hasa, kila mtu awe busy kama staff wa kpmg, delloite, pwc, ey.. etc...

Sijawai ona staff wa oil and gas company kama petrobrass au halliburton ana muda wa kuuzulia hata birthday parties, ila watumishi wa umma wana muda huo wengi tu.

Hawana targets kazi wanafanya kwa spidi ya kobe. Nilikuwaga mtumishi wa uma zamani kabla sijasepa. Maana ofisi watu wamekalia wanawaza posho, semina na majungu tu.

Niko upande wa magufuli, kuongeza mshahara kwa watu wasiozalisha sio sahihi, Japo watasema utumishi wa uma ni huduma. Wafike ubalozi wa marekani waone watumishi wa uma wa serikali ya marekani aka department of state walivyo busy. Hata simu zao binafsi hawazitumii wakiwa kaziniii.

Ili viwanda vije lazima tuige utamaduni wa walioendela au huawei kwa mafano.. ni kampuni ya serikali ya china.. fika pale jubelee tower posta.. uone staffs wa huawei wachina walivyo busy muds wa kazi
Kwa mawazo haya sidhani kama wewe ni mkweli au una uwezo wa kuelewa kinachoendelea kwenye sekta ya umma. Kama kweli unafikiri kwamba wafanyakazi sekta ya umma karibu wote ni wavivu/wazembe, basi lazima uwe katika kundi la wanafiki wa kisiasa waliopania kuhujumu nchi kwa manufaa binafsi. Tuige utamaduni wa walioendelea? Sahau. Tunaposema utawala wa CCM umevuruga mipangilio yote ya ufanisi nchini sijui kama unaweza kuelewa kitu. Ndio maana hawataki kusikia mabadiliko makini ya katiba.

Tafuta watumishi wa serikali/umma waliokuwa wakifanya kazi kwa juhudi, maarifa na kwa uaminifu maisha yao yote walipoishia kama walipona kufukuzwa kazi kabisa. Hata leo hii huko serikalini, fanya kazi kwa weledi mkubwa na kujituma hasa bila kupindisha kitu uone kama matokeo yatakuwa chanya. Halafu tafuta wanaofanikiwa kama ni wale wanaochapa kazi kikamilifu. Kama sio wale weledi wa kujikomba kwa mabosi. Uliza kuanzia Ikulu, utumishi, mawizarani kama "targets" zinafahamika na kuheshimiwa. Kama kuna mtumishi anathaminiwa kwa kutimiza vigezo hivyo.

Nchi kama Marekani kwanza kabisa zilijenga mfumo thabiti wa sekta ya umma unaohakikisha mafanikio yanapatikana kwa wote kwa kujituma kikazi, kutimiza malengo na kwa haki tu. Tena walipigana vita kadhaa na damu kumwagika ili kuhakikisha wanaandika mfumo (katiba) usioweza kuchezewa na mjinga yoyote. Usidanganye watu kwamba kufanya kazi kwa juhudi katika mazingira ovyo kama tuliyo nayo kunaweza kuleta tija kwa watu binafsi na taifa. Labda kwa vibaraka wa wanasiasa wa chama tawala pekee. Kwanza, hata hivyo vipimo makini vya ufanisi na tija hatuna. Nothing like a credible monitoring and evaluation system in TZ's public service. Sijui kama kuna wadanganyika wameamini kweli ipo siku wataarifiwa kwamba sasa uzalishaji umeongezeka hivyo "nawaongezea mshahara"!
 
Pamoja na kwamba watu wengi mna mbishia mleta UZI to me anayo point; Wafanyakazi wa serikali wengi wao ni wavivu sana, hawana malengo kabisa ya kile wanacho kifanya. Twendeni taratibu, nani ameisha wahi ona walimu wa shule za serikalini wapo wote kwa idadi yao saa 1:30 asubuhi!? Umeisha wahi sikia walimu wanasikitia wanafunzi wao kufeli mitihani yao kama wa private schools!? Nenda hospitali yoyote ya umma halafu angalia commitment za staff wale and then linganisha na wale au hao hao staff wakiwa huku ambako wengi wetu humu hua tunatibiwa. Wizarani na taasisi zake, kote tu, kila jambo linalo wenzekana leo kwa sekta binafsi kwa serikali unaweza subiri over one month. Namuunga mkono mleta UZI.
 
Najua wengi watachukia, ila ili hii nchi iendeleee lazima watu tufanye kazi. Navyosema kazi namaanisha kazi hasa, kila mtu awe busy kama staff wa kpmg, delloite, pwc, ey.. etc...

Sijawai ona staff wa oil and gas company kama petrobrass au halliburton ana muda wa kuuzulia hata birthday parties,
ila watumishi wa umma wana muda huo wengi tu.

Hawana targets kazi wanafanya kwa spidi ya kobe. Nilikuwaga mtumishi wa uma zamani kabla
sijasepa. Maana ofisi watu wamekalia wanawaza posho, semina na majungu tu.

Niko upande wa magufuli, kuongeza mshahara kwa watu
wasiozalisha sio sahihi, Japo watasema utumishi wa uma ni huduma. Wafike ubalozi wa marekani waone watumishi wa uma wa serikali ya marekani aka department of state walivyo
busy. Hata simu zao binafsi hawazitumii wakiwa kaziniii.

Ili viwanda vije lazima tuige utamaduni wa walioendela au huawei kwa mafano.. ni
kampuni ya serikali ya china.. fika pale jubelee tower posta.. uone staffs wa huawei wachina walivyo busy muds wa kazi

Kama mishahara yenyewe haiongezwi wacha watumishi wapumzike wapige soga
 
Nimewahi kufanya kazi ya mkataba na USA Peace corps, hawa watu ni more than smart!
 
kama unaweza kufanya kazi naweza kukuajiri kweli kwenye moja ya miradi yangu.. ila huko ni KPI tu
kama unawaza mshahara huku unachat ofisini kaa mbali kabisa

Kama umeweka KPI ni kwamba ninaweza kumaliza target zako (KPI) mapema kabla ya muda wa kazi kuisha na nikapata muda wa ku-chat ofisini na kusoma magazeti na kubishana kuhusu Manchester na Arsenal. Utanifanya nini nikifanya hivyo.
 
Kuna watu waajabu yaani unafananisha Manamba wa kampuni binafsi na watumishi wa umma
 
maisha ni ushindani kwa ujumla.

nyinyi ndio mnalirudisha nyuma hili taifa.. bila kujituma...na kuwa na competitive spirit huwezi endelea..

maisha ni ushindani.. hata wanyama wanashindana kugombea chakula msituni
Tatizo watanzania hawapendi kuambiwa ukweli,utendaji wa ofisi za serikali tunaujua,walitaka Rais awapetipeti na kuwasifia uongo wakati wananchi hawapati huduma stahiki kwa wakati sababu ya uvivu wa wafanyakazi wa serikalini,fanyeni kazi....asiefanya kazi asile.
 
Najua wengi watachukia, ila ili hii nchi iendeleee lazima watu tufanye kazi. Navyosema kazi namaanisha kazi hasa, kila mtu awe busy kama staff wa kpmg, delloite, pwc, ey.. etc...

Sijawai ona staff wa oil and gas company kama petrobrass au halliburton ana muda wa kuuzulia hata birthday parties, ila watumishi wa umma wana muda huo wengi tu.

Hawana targets kazi wanafanya kwa spidi ya kobe. Nilikuwaga mtumishi wa uma zamani kabla sijasepa. Maana ofisi watu wamekalia wanawaza posho, semina na majungu tu.

Niko upande wa magufuli, kuongeza mshahara kwa watu wasiozalisha sio sahihi, Japo watasema utumishi wa uma ni huduma. Wafike ubalozi wa marekani waone watumishi wa uma wa serikali ya marekani aka department of state walivyo busy. Hata simu zao binafsi hawazitumii wakiwa kaziniii.

Ili viwanda vije lazima tuige utamaduni wa walioendela au huawei kwa mafano.. ni kampuni ya serikali ya china.. fika pale jubelee tower posta.. uone staffs wa huawei wachina walivyo busy muds wa kazi
Fafanua hoja yako
 
Kwanza watumishi wa umma wafanyekazi kwa kujitolea, mwaka mmoja jkt miwili unajitolea serikali ndo unaingia uraiani, nchi yetu imechelewa sana kuendelea.
Acha ujinga na kukarili mambo.
Hao walioenda jkt wana kipi cha kutufundisha?
Wamefanya kipi spesheli ktk nchi hii?

Uzalishaji si maneno ya kisiasa tu
Kufanyeni kazi"
Kwa nyenzo zipi?
Kwa mazingira yapi rafiki?
Kwa uwekezaji upi uliofanya ktk taasisi za umma?
Kwa motisha ipi uliotoa?
 
KPI bado zina matatizo hapa Tanzania. Sheria zetu zinatambua sana Job description na hivyo KPI bado inaleta matatizo. Kesi karibu zote zinazohusu KPI waajiri wanashindwa maana haziendani na sheria ya kazi hasa Code of Good Practise.
Nashukuru kwa kupata point hapa...

Lakini ni wakati sasa serikali kuweka KPI's kwa wafanyakazi wa umma ili itusaidie kuongeza ufanisi na kukomesha wale wanaojifisha migongoni kwa wengine....
Mkuu unaonekana uko vema kwenye haya mambo ya KPI Plus sheria za kazi na code of good conduct....kuna uhusiano gani kati ya KPI na sheria za kazi? hebu nyanyambua NIPE SHULE MKUU...Ukimalizia na codes of good conduct nasubiri jibu Mkuu...

Section 15(1)(c) of Employment and Labour Relation Act, No. 6 of 2004 (ELRA) inasema kila mwajiriwa lazima awe na “Job Description”. Hakuna section inayosema kila mwajiriwa lazima awe na “KPI”.

Section 15(1)(c) of ELRA inasema mwajiri hawezi kukubadilishia “Job Description” bila wewe kuiridhia. Analazimika kwanza akuletee na wewe ujadili cha kuondoa au kuongeza kisha mnaikubali wote. Hivyo, unapokuwa na “KPI” mwajiri hapaswi kuileta kwa jinis anavyotaka bali lazima aombe ruhusa ya mwajiriwa ili aikubali hiyo “KPI” maana kwa uzoefu ni kwamba “KPI” ni kiwango tu cha kazi zilizoorodheshwa kwenye “Job Description” na sin je ya hapo.

Ukija kwenye kanuni za sheria hizi ziko zinaitwa “Employment and Labour relations (Code of Good Practice) Rules, 2007”. Kifungu cha 17(2) kinasema “Although the employer has the managerial prerogative to set performance standards, the standards shall not be unreasonable”.

Hivyo, usidhani kwamba eti bosi wako anaweza tu kujitungia kwamba leo nesi umehudumia wagonjwa 20 sasa mimi kama bosi wako nakupangia “KPI” ya kuhudumia wagonjwa 40! Hapa ukimfukuza kazi mtu kwa underperformance kama mnavyotaka, inabid wewe mwajiri ukathibitisha mahakamani kwamba kumpangia wagonjwa 40 ilikuwa reasonable. Hapa ndipo waajiri karibu wote nchini wamekuwa wakishindwa kwenye kesi hizi za “KPI”.

Hao mnaowataja kwamba wamefaulu zoezi la “KPI” si kweli kwamba wamefaulu. Kinachotokea ni kwamba wanalipa mishahara mikubwa wafanyakazi wao kisai kwamba wafanyakazi wenyewe wanajitesa kukaa hata usiku kufanya kazi ili wamalize kazi wapate hela nyingi. Lakini akiibuka mfanyakazi wa huko akawashitaki anaweza kuwashinda kesi kirahisi kwa kigezo kilekile cha “reasobability”.

Natumaini mmenielewa mnaopinga na mnaopenda “KPI” iwekwe serikalini. Namalizia tena, kikubwa kazini ni "Job Description" ambayo naamini hata mliomo humu, asilimia zaidi ya 90 hamna "Job Description" hapo kazini kwenu.

Hujui hata maana ya mkataba wa ajira , hujui consequences za kufukuza watumishi wote
Kwa sasa KPI hazifai kwa kuwa mazingira ya kazi siyo wezeshi
NAUNGA MKONO HOJA, FUKUZA WOTE.
CHONDECHONDE MUHESHIMIWA RAISI ANZA NA TANESCO KAMA PILOT AMA MODELI YA ZOEZI HILI KWA MASHIRIKA NA TAASISI ZOTE.

Mtu kama ni mvivu sheria za kazi ziko wazi, ni kumchukulia hatua....msingi wa kusema watu hawatendi vyema

hao wafanyakazi wa makampuni uliyoyataja packages zao zikoje? mazingira yao ya kazi yakoje? Je wanapata nyenzo zote za kazi kwa wakati?
 
Section 15(1)(c) of Employment and Labour Relation Act, No. 6 of 2004 (ELRA) inasema kila mwajiriwa lazima awe na “Job Description”. Hakuna section inayosema kila mwajiriwa lazima awe na “KPI”.

Section 15(1)(c) of ELRA inasema mwajiri hawezi kukubadilishia “Job Description” bila wewe kuiridhia. Analazimika kwanza akuletee na wewe ujadili cha kuondoa au kuongeza kisha mnaikubali wote. Hivyo, unapokuwa na “KPI” mwajiri hapaswi kuileta kwa jinis anavyotaka bali lazima aombe ruhusa ya mwajiriwa ili aikubali hiyo “KPI” maana kwa uzoefu ni kwamba “KPI” ni kiwango tu cha kazi zilizoorodheshwa kwenye “Job Description” na sin je ya hapo.

Ukija kwenye kanuni za sheria hizi ziko zinaitwa “Employment and Labour relations (Code of Good Practice) Rules, 2007”. Kifungu cha 17(2) kinasema “Although the employer has the managerial prerogative to set performance standards, the standards shall not be unreasonable”.

Hivyo, usidhani kwamba eti bosi wako anaweza tu kujitungia kwamba leo nesi umehudumia wagonjwa 20 sasa mimi kama bosi wako nakupangia “KPI” ya kuhudumia wagonjwa 40! Hapa ukimfukuza kazi mtu kwa underperformance kama mnavyotaka, inabid wewe mwajiri ukathibitisha mahakamani kwamba kumpangia wagonjwa 40 ilikuwa reasonable. Hapa ndipo waajiri karibu wote nchini wamekuwa wakishindwa kwenye kesi hizi za “KPI”.

Hao mnaowataja kwamba wamefaulu zoezi la “KPI” si kweli kwamba wamefaulu. Kinachotokea ni kwamba wanalipa mishahara mikubwa wafanyakazi wao kisai kwamba wafanyakazi wenyewe wanajitesa kukaa hata usiku kufanya kazi ili wamalize kazi wapate hela nyingi. Lakini akiibuka mfanyakazi wa huko akawashitaki anaweza kuwashinda kesi kirahisi kwa kigezo kilekile cha “reasobability”.

Natumaini mmenielewa mnaopinga na mnaopenda “KPI” iwekwe serikalini. Namalizia tena, kikubwa kazini ni "Job Description" ambayo naamini hata mliomo humu, asilimia zaidi ya 90 hamna "Job Description" hapo kazini kwenu.
Hii ndo inaitwa Great think....to be logical Criticall,analytical coherent...
Ngoja nikuulize swali....je na ile ya kupangiwa any other duties BY YOUR SUPERIOR ...ambapo ipo kwenye job description haiwezi kuingia kwenye KPI?
 
Kuna tofauti ya kuwa busy na kuwa productive,, sio kila aliye busy ni productive. Na kuna watumishi wengi wa umma ambao ni very productive kwenye sehemu zao za Kazi
 
NAUNGA MKONO HOJA, FUKUZA WOTE AJIRI UP YA TENA KWA MIKATABA YA MIAKA MIWILIMIWILI TU, NA KUONGEZA MKATABA MWENGINE UFANISI UANGALIWE.
CHONDECHONDE MUHESHIMIWA RAISI ANZA NA TANESCO KAMA PILOT AMA MODELI YA ZOEZI HILI KWA MASHIRIKA NA TAASISI ZOTE.
Ili swala nilishawahi lifikiria siku nyingi mno. Nadhani ajira zikiwa za mkataba zitaondosha ile hali ya waajiriwa kubweteka na kuanza kutengeneza network za kifisadi. Watu waangaliwe jinsi gani wapo active ku deliver na kufikisha goals za mwaka mzima. Isiwe watu wanaenda kazini tu kama wajibu halafu output ni 0% hasara tupu.
 
Hii ndo inaitwa Great think....to be logical Criticall,analytical coherent...
Ngoja nikuulize swali....je na ile ya kupangiwa any other duties BY YOUR SUPERIOR ...ambapo ipo kwenye job description haiwezi kuingia kwenye KPI?
NASUBIRI JIBU HAPA
SubiriJibu
 
Back
Top Bottom