MAGUFULI chapakazi, tutakuhukumu sisi wanyonge siyo Wanasiasa vigeuvigeu.

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
Naanza kuyakumbuka Maneno ya mwanazuoni na mwanasiasa Prof. KITILA MKUMBO. Baada ya Uchaguzi mkuu mwaka jana uliopelekea Dr. John Pombe Magufuli kuchaguliwa kuwa Rais wa awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Prof. Kitila Mkumbo akihojiwa na kituo kimoja cha Television nchini alisema "WAPINZANI WAKIFANYA MAZOEA YA KUTUMIA MADHAIFU YA CCM KUJIIMARISHA, AWAMU YA TANO WANAWEZA KUWA NA WAKATI MGUMU"

Kwa muda mrefu sana makundi takribani yote ya watanzania wakiwemo Wanasiasa, vijana, Wazee, Walemavu, Wafanyakazi, Wanyonge(wale wa kipato cha chini) na mengine mengi waliimba nyimbo mbalimbali za aina ya rais wanayemtaka kuwa ni:
1. Rais ambaye atadhibiti rushwa
2. Rais ambaye atawajali watu wa kipato cha chini
3. Rais atakayesimamia nidhamu ya kazi katika taasisi za Umma
4. Rais ambaye hataruhusu matumizi yasiyo ya lazima serikalini.
5. Rais ambaye Hatakuwa na safari za mara kwa mara nje ya nchi kwa sababu zinakuwa za gharama kubwa.

Watanzania tukaenda mbali sana tukasema ikibidi tunahitaji RAIS DIKTETA ili kuyasimamia hayo mambo niliyaainisha hapo juu. Walioongoza DUA hizi kwa mwenyeji Mungu walikuwa ni Wanasiasa na hasa wa vyama vya Upinzania hususan Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA).

Baada ya Rais Dr. John Pombe Magufuli kuanza kazi yake na hasa alipoamua kutekeleza kwa vitendo ahadi yake aliyoiahidi Bungeni ya KUTUMBUA MAJIPU, Kauli nyingi sana zimesewa na Wapinzani ndani na nje ya Bunge. Kauli ambazo zinapingana kabisa na DUA zetu(WAPINZANI WAMEKUWA VIGEUGEU).
Baadhi ya kauli hizo ni pamoja na ile ya:
1. Wafanyabiashara waliofadhili CHADEMA katika uchaguzi mkuu wananyanyaswa katika suala zima la kuwashuggulikia wakwepa kodi.
2. Rais Magufuli aende nje asikae tu ofisini , aende akutane na rais POTINI wa Urusi.
3. Wafanyakazi wanafukuzwa hovyo na hawapewi nafasi ya kujitetea.
4. Serikali ya Magufuli haifuati utawala wa sheria(Rais ni Dikteta).

KUMBUKUMBU: Ni wapinzani hao hao waliosema Magufuli anatekeleza Ilani ya UKAWA pale alipoanza kuonesha kwa vitendo kuwa ana nia ya dhati ya kujibu DUA za muda mrefu za Watanzania hasa wale wa kipato cha chini.
Kauli hizi za ukigeugeu wa wanasiasa na hasa wapinzani ni wazi MANENO YA PROF. KITILA MKUMBO yanatimia. Wamekosa hoja ma watapata wakati mgumu.

RAIS ASHIKILIE HAPO HAPO, TUTAMHUKUMU SISI WATANZANIA WANYONGE NA SIYO WANASIASA VIGEUGEU.
 
Andiko zuri sana hili. Wapinzani hoi bin taaban.
 
kuanzisha thread mwenyewe na kujijibu mwenyewe ni sawa na kujitekenya mwenyewe na kucheka mwenyewe.
Ni muendelezo wa kuunga mkono wachangiaji wengine. Kuanzisha mada hakunifungi mimi kutochangia. Shirikisha ubongo mkuu.
 
Binaadamu hawana jema wakita hili na kulipata kesho watageuza tena na kuliona baya bora lingekua hivi
Wanasiasa sio watu wa kuamimi ni wakusililza tu wamachosema na kuachananao
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom